HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

December 09, 2019

Askofu Shimbe ataka watu kubuni miradi ya kiuchumi

Askofu Mkuu wa Kanisa la EAGT Jimbo la Magu, Mkoa wa Mwanza, Cosmas Shimbe (kulia) akimuombea mmoja wa waumini wa kanisa hilo, katika Ibada Takatifu iliyofanyika EAGT Bethel Kisesa wilayani humo, mwishoni juzi. Katika Ibada hiyo iliyohudhuriwa na mamia ya waumini, Askofu Shimbe alihimiza watu kufanyakazi ili kujinasua na dhoruba ya umasikini. (Picha na Sitta Tumma).
Kwaya.
Kwaya ya vijana.
Waumini wa Kanisa la EAGT Bethel Kisesa, Wilaya ya Magu mkoani Mwanza, wakiwasikiliza wanakwaya wa vijana wa kanisa hilo, huku Askofu Shimbe akipokea zawadi kutoka kwa kijana aliyetokea Musoma, Mkoa wa Mara.
Waumini wa Kanisa la EAGT Bethel Kisesa, Wilaya ya Magu mkoani Mwanza, wakiwasikiliza wanakwaya wa vijana wa kanisa hilo, huku Askofu Shimbe akipokea zawadi kutoka kwa kijana aliyetokea Musoma, Mkoa wa Mara.

Na Mwandishi Wetu, Magu
ASKOFU Mkuu wa Kanisa la EAGT Jimbo la Magu, Mkoa wa Mwanza, Cosmas Shimbe, ameshauri Watanzania kuwa wabunifu katika kuanzisha miradi ya uzalishaji mali.

Amesema umasikini utaondoka iwapo kila mtu atafanyakazi kwa bidii, maarifa na kujituma kama inavyohimizwa na Mwenyezi Mungu kupitia maandishi yake matakatifu.

Askofu Shimbe amesema hayo alipoongoza Ibada Takatifu kwenye Kanisa hilo, Bethel Kisesa, akisema kazi inamuwezesha mtu kujiweka kando na tatizo la umasikini..

Amesema tatizo la umasikini lazima lipigwe vita kwa watu wakiwamo vijana na wanawake, kutumia vizuri fursa zinazowazunguka katika kuanzisha miradi ya kiuchumi.

"Lazima ufanye kazi. Unapokuwa kanisani hapa ukiwa na pesa yako, unapigwa neno zuri na ukitoka na wewe unakwenda kupiga supu.

"Tufanyekazi. Wanawake walalamishi ni wasiofanyakazi, mara ooh mume hajali familia. Fanyakazi, mume alete na mwanamke aleta mnakusanya nguvu. Siyo uwe tegemezi," amesema Askofu Shimbe.

Kulingana na kiongozi huyo wa kiroho, Kumbukumbu la Tolati Sura ya 8 mstari wa 18 Mungu anataka mtu afanyekazi ili afanikiwe.

Kwamba, katika maandiko hayo matakatifu, Paul naye anasema anafanya kazi usiku na mchana ili nisiwaelemee watu.

"Kila mtu aliyejaliwa akili na afanyekazi ili upate fedha. Siyo kuona mtu wareti imejaa kumbe ndeni kuna karatasi rundo," amesema Askofu Shimbe huku waumini wakiangua kicheko kanisani.

Askofu Mkuu huyo wa EAGT Jimbo la Magu amekemea tabia ya baadhi ya watu kuchagua kazi za kufanya, badala yake ametaka watu wafanyekazi hata ya kuuza mkaa au vitumbua magengeni, ili kujipatia fedha.

No comments:

Post a Comment

Pages