Na Mwandishi Wetu
KLABU ya Azam FC leo imeingia mktaba na Ali Tuli kuwa Ofisa Masoko wa klabu hiyo.
Tuli atakuwa na jukumu la kuitangaza timu 'Kui Brand' kuipatia masoko yakiwemo ya kuuza vifaaa vya michezo vya Azam FC.
"Tunatarajia kwa uzoefu wake tutaweza kupata mafanikio makubwa katika nyanja ya masoko kwa klabu yetu.
"Lakini
pia moja ya jukumu lake ni kuhakikisha klabu inapata wadhamini wengi,
jambo ambalo litaiwezesha klabu kupunguza gharama za uendeshaji."
amesema Jafari Idd Ofisa habari wa Azam FC.
Idd
ameongeza kuwa kesho kikosi chao kitakuwa na mchezo wa kirafiki dhidi
ya Dar City, ambayo inashiriki Ligi Daraja la Pili (SDL).
Mchezo huo unatarajiwa kulindima katika Dimba la Uhuru jijini Dar es Salaam kuanzia majira ya saa 10:00 za jioni.
"Leo
pia Uongozi wa Azam tumekaa na mchezaji wetu raia wa Burundi Suleiman
Ndikumana tuliyemsajili msimu huu, amekuwa akiandamwa na majeruhi ya
muda mrefu hivyo tumeamua kuvunja mkataba kwa makubaliano ya pande zote
mbili.
"Ni wazi kuanzia
sasa hatutakuwa na Ndikumana kama mchezaji wa Azam tumemalizana nae,
tayari amerejea kwao Burundi hivyo nafasi yake Mwalimu ndio ataamua kama
atahitaji mtu wa kuiziba basi tutafanya hivo. " ameongeza Idd.
No comments:
Post a Comment