NA
TIGANYA VINCENT
MKUU wa Wilaya ya Uyui,
Gift Msuya, amewaagiza Watendaji wa Vijiji kushirikiana na Jeshi la
Akiba(Mgambo) kuwakamata wakulima wote ambao hawakulima zao hilo licha ya
kuchukua mbegu na dawa za kuua wadudu waharibifu wa pamba msimu uliopita.
Aliagiza kuchukua hatua
hiyo baada ya wakulima hao kushindwa kulima pamba na wengine kutorosha pamba na
kwenda kuuzia maeneo mengine jambo ambalo limesababisha kushindwa kulipa deni
lao la shilingi milioni 53 wanazodaiwa na Kampuni za Kahama Cotton Company
Limited na Kahama Oil Mill wiki hii.
Msuya alitoa kauli hiyo
jana wakati wa ziara ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri kwenye kampeni
yake ya kuhamasisha kilimo ikiwemo cha pamba katika Kijiji cha Migungumalo.
Alisema alisema deni hilo
wanaodaiwa wakulima limesababisha Kampuni hizo kukataa kulipa deni la ushuru wa
Halmashauri ya Wilaya ya Tabora wanaodaiwa wa shilingi milioni 46 zinazotokana
na mauzo ya kilo milioni 1.2 za msimu uliopita.
Msuya alisema
uchelewashaji wa fedha hizo kutoka Kampuni hizo kwa ajili ya ushuru wa
Halmashauri umesababisha kukwamisha baadhi ya shughuli za maendeleo ikiwemo za
ujenzi wa vyumba vya madarasa.
Kwa upande wa Mkuu wa
Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri amemuagiza Afisa Ushirika kuorodhesha wakulima
wote wanaodaiwa na kukabidhi majina ya wakulima hao ambao hawataki kulipa ili
hatua zichukuliwe dhidi yao.
Alisema haiwezekani
mkulima achukue mbegu bila kupanda na kuacha bila kudaiwa na kuongeza kuwa ni
vema ikiwezekana kwa yule mwenye mifugo ataoa ili kulipa deni.
Katika hatua nyingine
Mkuu huyo wa Wilaya alisema kwa mujibu wa Sheria ndogo ndogo za Halmashauri ya
Wilaya ya Tabaora kila kaya ni lazima ilime ekari tatu za mazao ya chakula na
ekari tatu za mazao ya chakula.
Alisema asie tekeleza
jambo hilo anavunja Sheria na hatua kali dhidi yake zitachukuliwa.
No comments:
Post a Comment