HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

December 17, 2019

TMA: MVUA ITAENDELEA, CHUKUA TAHADHARI

Meneja wa Utabiri kutoka Kituo Kikuu cha Utabiri cha Mamlaka ya Hali ya Hewa, Samuel Mbuya.


Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa, Dk. Agnes Kijazi.


Na Irene Mark

MAMLAKA ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), imesema ongezeko la mvua zinazoendelea kunyesha jijini Dar es Salaam na baadhi ya mikoa ya Pwani ni matokeo ya kuimarika kwa ukanda wa mvua kwenye nchi yetu.

Akizungumza na Habari Mseto Blog, jijini Dar es Salaam leo Desemba 17, 2019; Meneja wa Huduma za Utabiri kutoka TMA, Samuel Mbuya alisema hali hiyo imetokana mkondo wa baridi kwenye ncha ya Kusini mwa Bara la Africa.

Alitaja baadhi ya mikoa iliyopata ongezeko hilo la mvua kuwa ni Dar es Salaam, Pwani, Tanga, Kaskazini mwa Morogoro, Pemba na Unguja.

Maeneo mengine ni mikoa ya Kanda ya Kati ambayo ni Singida na Dodoma huku akisisitiza kwamba mvua hizo zitafikia ukomo leo alasiri.

Kwa mujibu wa Mbuya, wakazi wa maeneo yaliyopata ongezeko la mvua wanashauriwa kuendelea kuchukua tahadhari ili kuepuka athari za maji.

"Lakini pia tuanatoa msisitizo kwa wakazi wa maeneo tuliyoyaweka kwenye angalizo la mvua kubwa kuchukua tahadhari ya mafuriko.

"...Maeneo hayo ni mikoa ya Iringa, Njombe, Rukwa, Mbeya, Ruvuma, Mtwara na Lindi. Hawa wanatakiwa kuzingatia angalizo la mvua kubwa itakayonyesha kuanzia leo," alisema Mbuya.

Hata hovyo ameahidi kuendelea kutoa taarifa za hali ya mvua kila wakati kadri wanavyozipokea kutoka kwenye mifumo yao.

No comments:

Post a Comment

Pages