HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

December 17, 2019

MASHINDANO YA GOFU MORO YAMALIZIKA MCHARO WA TPC AIBUKA MSHINDI

 Mchezaji Ally Mcharo wa Klabu ya TPC akipokea kikombe cha ushindi  kutoka kwa  Mwenyekiti wa Klabuya lugalo  Brigedia jenerali Mstaafu Michael Luwongo Mstaafu aliyekuwa mgeni rasmi baada ya kupiga mikwaju Gross 160  kwa siku zote mbili za Mashindano yaliyofanyika katika Uwanja wa Gymkhana Morogoro.
Wachezaji  wa gofu kutoka kushoto ni Angel Eaton wa Lugalo Edna Chiwinga wa Morogoro na wa kwanza kulia ni Hadija Selemani wakielekezana jambo wakati wa Mashindano yaliyofanyika katika Uwanja wa Gymkhana Morogoro mwisho wa wiki.
Mchezaji  Vicky Elias  wa Klabu ya Lugalo  akipokea kikombe cha ushindi  wa kwanza  kwa waknawake kutoka kwa  Mwakilishi kutoka Orynx  Cira  Muhele baada ya kupiga mikwaju 155  kwa siku zote mbili za Mashindano yaliyofanyika katika Uwanja wa Gymkhana Morogoro.
Mshindi wa pili wa  mashindano ya wazi ya Gofu Morogoro open Zacharia Edward wa  Klabu ya Lugalo  akipokea kikombe cha ushindi  wa pili kutoka kwa  Mwenyekiti wa Klabu ya lugalo aliyekuwa Mgeni rasmi katika shereza za utoaji zawadi na Kufunga  Mashindano yaliyofanyika katika Uwanja wa Gymkhana Morogoro mwisho wa wiki.
Mshindi wa pili wa  mashindano ya wazi ya Gofu Morogoro Open Zacharia Edward wa  Klabu ya Lugalo  akipokea kikombe cha ushindi  wa pili kutoka kwa  Mwenyekiti wa Klabu ya lugalo aliyekuwa Mgeni rasmi katika shereza za utoaji zawadi na Kufunga  Mashindano yaliyofanyika katika Uwanja wa Gymkhana Morogoro mwisho wa wiki.
 

Na Mwandishi Wetu

Mashindano ya wazi ya gofu Morogoro yamemalizika huku mchezaji Ally Mcharo wa Klabu ya TPC akiibuka na ushindi baada ya kupiga mikwaju Gross 160  kwa siku zote mbili za Mashindano yaliyofanyika katika Uwanja wa Gymkhana Morogoro.

Mshindi wa pili ni Zacharia Edward wa lugalo ambaye alipiga Mikwaju 161 huku upande wa Mikwaju ya Jumla  Net kwa Divisheni A Mshindi ni  Michael Mtweve wa  Mufindi  aliyepiga  mikwaju ya Jumla 155 akifuatiwa na Maurus Kajuna  wa Lugalo.

Katika Divisheni  B Mshindi wa Kwanza kwaa Mikwaju ya jumla ni  Amadi Rajabu wa Dar es salaam Gymkhana  akifuatiwa na Teddy Kalinga wa Lugalo huku Divisheni C Mshindi ni  Rory Mickllem wa Morogoro Gymkhana  akifuatiwa na Musa Joseph wa Mufindi.

Kwa upande wa Wanawake Mshindi ni Vicky Elias wa Lugalo akifuatiwa na Joyce Warega naye wa Lugalo  huku kwa Upande wa watoto ambao ni wa Morogoro pekee walichuaana na Mshindi ni Robert Colnelius huku mshindi wa pili ni  Rajabu Omary na aliyepiga mpira mrefu  ni Ally Mcharo na Hadija Selemani na waliopiga mpira jirani ni Zacharia Edward na Edna Chiwinga.

Akifunga Mashindano hayo Mgeni rasmi ambaye pia ni mwenyekiti wa Klabu ya Golf ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania Brigedia Jenerali Michael Luwongo Mstaafu alitaka klabu kuendeleza ushirikiano wa karibu na kuelekea kwenye maridhiano ya wachezaji wanachama wa klabu moja kuruhusiwa kucheza katika Klabu Nyingine bila Gharama.

“ Ili kuendeleza Mchezo hakuna Sababu mwanachama kulipishwa kila Sehemu ikiwa ni familia Moja hivyo Lugalo itaanza na Morogoro Gymmkhaana na Bilaa Shaka vilabu vingine navyo vinaweza kuunga Mkoano” Alisema Brigedia Jenerali Luwongo.

Pia alisema katika Mpango wa kukuza Vipaji Lugalo inatarajia kufikisha Idadi ya watoto 70 hivyo  vilabu vingine navyo vianze kwa wananchama kwenda klabu zao na watoto wao kabla ya kushawishi watoto wengine iii kuibua vipaji vipya.

Aidha alisema Lugalo ipo tayari kutoa usaidizi wa kufundisha walimu wa Michezo katika mashule ya serikali iwapo Serikali itaamua na kuwaelekeza kwani ni klabu ya Jeshi kutoka Serikalini ni maelekezo naa Klabu iko Tayari muda Wote.

Kwa upande wake mwakilishi wa Chama cha gofu Tanzania Enock Magile amepongeza vilabu Vyote vilivyoandaaa Mashindano Mwaka 2019 na kuongeza kuwa Kalenda Kwa Mwaka 2020 imekamilika ni matumaini ya TGU mashindano yatafanyika kwa viwango zaidi ya Mwka uliopita.

Naye  makamu mwenyekiti wa Morogoro Louis Roussos  alishukuru Lugalo na wachezaji wengine kwa ushirikiano ikiwemo wa kiufndi katika kufanikisha mashindano hayo ambayo yanafunga mwaka kwa mujibu wa kalenda ya TGU.

No comments:

Post a Comment

Pages