HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

December 06, 2019

Madereva zaidi 200 wajiunga na mfumo wa inDrive

Na Mwandishi Wetu
 
MADEREVA zaidi ya 200 wa Jijini Mbeya
wamejiunga katika mfumo wa Mtandao wa Kimataifa unaotoa huduma za usafiri  (inDriver).

Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari jana ...ilisema kuwa Mtandao huo wa  kimataifa unatoa huduma za usafiri wenye makao makuu yake Mountain View-California, Marekani na unatumiwa na watu zaidi ya milioni 35 kupitia miji zaidi ya 30.

"Mbeya ni jiji la pili kuzindua mfumo huu wa usafirishaji wa inDriver, baada ya Arusha. Ambapo  umeweza kuunganisha zaidi ya madereva 200 wa mjini Mbeya, na wengine wengi wanaendelea kusajiliwa kila siku. Katika hatua za awali,mfumo huu wa inDriver  hautatoza  madereva kiasi chochote cha kamisheni," Ilifafanua.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, watumiaji wa mtandao huo wanaweza kupanga bei ya usafiri kwa uhuru wakati madereva wanaweza kuchagua njia (route) zenye faida na wanazozipendelea wao wenyewe. 

Ilisema kuwa Mfumo wa program hiyo unazuia kuongezeka kwa gharama kama vile kukiwa na foleni, na historia ya maombi ya safari kitu ambacho ni tofauti na makampuni mengine ambayo yanaongeza bei.

"Mfumo huu wa usafirishaji unaruhusu abiria kuweka nauli zao wenyewe kwa njia watakayoichagua na kuipendelea. Madereva wa karibu ambao wanapata taarifa ya kupata usafiri huwa wana chaguzi tatu," ilieleza taarifa hiyo

Taarifa hiyo ilizitaja chaguzi hizo kwa madereva ni kukubali nauli inayotolewa, kupuuza nauli inayotolewa au kufanya mazungumzo ili nauli iongezeke. 

Ilisema kuwa abiria anaweza kuchagua aina ya gari anayohitaji au bajaji.

Taarifa aliongeza kuwa kitu pekee cha tofauti katika mfumo huu wa inDriver ni kwamba madereva hawajasajiliwa moja kwa moja (automatically) kwa watumiaji. 

"Abiria anachagua dereva atakayeona anafaa zaidi na aina ya vipaumbele vyenye umuhimu kwake binafsi kama vile gharama za  nauli, kiwango cha dereva, makadirio ya muda wa kuwasili na aina ya gari litakalotumika.

Iliongeza kuwa mfumo huo wa inDriver una chaguo la kumfanya mtumiaji asafiri salama huku abiria anaweza akatumia GPS (mfumo wa kuonesha mahala mtu alipo) ya maeneo ya safari kwa wakati halisi kutoka kwenye programu  kwa mawasiliano kwa watu wanaoaminika.

"Kusafiri na inDriver kunaweza kufanyika kupitia mipaka ya jiji la Mbeya na vitongoji vya karibu.Kwa sasa, malipo yanaweza kufanyika hapo kwa hapo, pia inaruhusu kupunguza gharama za safari, kama malipo yakifanyika kupitia kadi kutakuwa na makato kiasi," ilieleza
  
Taarifa hiyo ilisema kuwa, abiria anaweza kuupakua mfumo huu wa  inDriver bure kutoka Google Play Store and AppStore.

No comments:

Post a Comment

Pages