Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, wakati akiwasili kwenye Mradi wa Ujenzi wa Machinjio ya Kisasa, Vingunguti jijini Dar es Salaam, Desemba 3, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, akifafanuliwa jambo na Mshauri wa Mradi wa Ujenzi wa Machinjio ya Kisasa Vingunguti, Henry Mwoleka, wakati alipokagua mradi huo, Desemba 3, 2019, jijini Dar es Salaam.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, akikagua Mradi wa Ujenzi wa Machinjio ya Kisasa, yaliyopo Vingunguti jijini Dar es Salaam.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, akifafanuliwa Mkandarasi wa Mradi wa Ujenzi wa Machinjio ya Kisasa
Vingunguti, Mhandisi Elisante Ulomi, wakati alipokagua mradi huo,
Desemba 3, 2019, jijini Dar es Salaam.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, akizungumza na Afisa Mfawidhi wa Machinjio Vingunguti, Jihadhari Mgeni, wakati alipokagua machinjio hayo, Desemba
3, 2019, jijini Dar es Salaam.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, akioneshwa jambo na Afisa Mfawidhi wa Machinjio
Vingunguti, Jihadhari Mgeni, wakati alipokagua machinjio hayo, Desemba
3, 2019, jijini Dar es Salaam.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, akizungumza na wananchi, baada ya kukagua Machinjio ya zamani yaliyopo Vingunguti jijini Dar es Salaam, baada ya kutembelea Mradi wa Ujenzi wa Machinjio ya Kisasa Vingunguti, Desemba 3, 2019.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, akizungumza na wananchi, baada ya kukagua Machinjio ya zamani yaliyopo Vingunguti jijini Dar es Salaam, baada ya kutembelea Mradi wa Ujenzi wa Machinjio ya Kisasa Vingunguti, Desemba 3, 2019.
Na Mwandishi Wetu
WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa amemtaka mkandarasi anayejenga machinjio ya kisasa ya
Vingunguti jijini Dar es Salaam ahakikishe kwamba anakamilisha ujenzi huo mwishoni
mwa mwezi huu kama alivyoamriwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli.
Akizungumza
mara baada ya kukagua ujenzi huo leo (Jumanne, Desemba 3, 2019), Mheshimiwa
Majaliwa amesema amefurahishwa na hatua ya mkandarasi huyo ambaye ni Shirika la
Nyumba la Taifa (NHC) ya kuongeza idadi ya watalaam na mafundi ili kuhakikisha
kwamba kazi hiyo inafanyika haraka na kukamilika kwa wakati ulioamriwa na Rais
Magufuli yaani Desemba 30, mwaka huu.
Amesema
amefurahi pia kuona kwamba mkandarasi huyo ameamua kufanya kazi usiku na
mchana, hatua ambayo imeongeza kasi ya ujenzi huo na anaamini kuwa kazi hiyo
itakamilika kwa wakati.
Mheshimiwa
Majaliwa amemtaka Mshauri Mwelekezi wa mradi huo ambaye ni M/SCONS
AFRIKA LIMITED na FB Consultant wa Dar es Salaam asimamamie kwa
karibu ili kujiridhisha kuwa maelekezo yote yaliyopo
kwenye michoro ya ujenzi huo yanazingatiwa na mkandarasi.
Amesema
Serikali imeamua kujenga machinjio hayo ya kisasa ya Vingunguti baada ya
kugundua kwamba wafanyabiashara wa mifugo na mazao yake katika
machinjio hayo, walikuwa wakifanya kazi zao kwenye mazingira duni
na kwamba nyama iliyokuwa ikitoka kwenye machinjio hayo ilikuwa
haikubaliki kwenye soko la nje ya nchi.
“Uamuazi
wa Serikali kujenga machinjio haya, utaifanya nyama inayotoka hapa ikubalike
kwenye masoko ya nje ya nchi, hatua ambayo itaongeza mzunguko wa fedha kwenye
eneo hili wakati Serikali na Manispaa watanufaika kwani kutakuwa na ongezeko la
makusanyo ya kodi,” aliongeza Mheshimiwa Majaliwa.
Waziri
Mkuu pia ameuagiza uongozi wa Mkoa wa Dar es Salaam pamoja na Manispaa ya Ilala
wafanye mazungumzo na uongozi wa Shirika la Reli Tanzania (TRC) ili ijengwe
reli ya mchepuko kutoka reli ya kati kwenda kwenye machinjio ya Vingunguti ili
mifugo iingizwe moja kwa moja kwenye machinjio hayo badala ya kuteremshiwa Pugu
halafu ikapelekwa kwa magari.
Amewahakikishia
wafanyabiashara wote wanaoendesha shughuli zao kwenye machinjio hayo kuwa
ujenzi wa machinjio ya kisasa ya Vingunguti hautawafanya wapoteze
fusa zao za biashara au kuajiriwa kwenye eneo hilo kwani machinjio
hayo yatafungua fursa zaidi za biashara na ajira kwao.
Amewaagiza
Mkuu wa Wilaya ya Ilala na Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala wahakikishe kwamba
wanaushirikisha uongozi wa wafanyabiashara wa mifugo na mazao yake wa
Vingunguti ili wanachama wao wenye sifa za kuajiriwa, waajiriwe na pia wawaandalie
mazingira ya kufanya biashara mbalimbali karibu na machinjio hayo.
Akizungumzia
soko na bei duni ya ngozi za mifugo nchini, Waziri Mkuu amekemea tabia ya
wafugaji ya kuweka alama kwenye ngozi za mifugo yao hasa ng’ombe kwani kufanya
hivyo kunashusha thamani ya ngozi za Tanzania na badala yake amewataka waweke
alama za hereni kwenye masikio ya mifugo yao ili kulinda ubora wa ngozi za
mifugo yao.
Amesema
Serikali tayari imekwishampata mwekezaji kutoka Misri ambaye amekubali kuwekeza
kwenye kiwanda cha ngozi cha Mwanza hatua ambayo italihakikishia Taifa soko la
ngozi.
Mapema, akitoa taarifa kwa
Waziri Mkuu, Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala, Jumanne Shauri amesema ujenzi wa
machinjio hayo ulianza Julai 8, mwaka huu na mkandarasi alitakiwa akamilishe
ujenzi huo ifikapo Januari 6, 2021. Amesema kufuatia agizo la Rais Magufuli
alilolitoa Septemba 16, mwaka huu, ujenzi huo unatakiwa ukamilike ndani ya miezi
mitatu yaani ifikapo Desemba 31, 2019.
Bw.
Shauri amesema awamu ya kwanza ya ujenzi wa mradi huo itagharimu
sh. 12, 498,916,063.00 ambapo sh. 8,528,486,470.00 ni ruzuku kutoka
Serikali Kuu na sh. 3, 970,429,593.00 zimetokana na mapato ya ndani ya
Halmashauri na kwamba ujenzi wa mradi huo kwa sasa umefikia asilimia 60.
Akisoma
risala ya Ushirika wa Wafanyabiashara ya Mifugo na Mazao
yake wa Vingunguti (UWAMIVI), Mwenyekiti wao, Bw. Joel Meshaki
aliiomba Serikali iwaandalie wafanyabiashara hao eneo mbadala
la kufanyia shughuli zao ili ajira yao isipotee.
Alipendekeza
kwa Waziri Mkuu maeneo matatu yaliyoko karibu eneo hilo, ambayo
yangewafaa wafanyabiashara hao wakati watakapoondoka kwenye maeneo
yao sasa yanapojengwa machinjio ya kisasa kuwa ni Dampo la zamani ambalo kwa
sasa halitumiki, eneo la Wizara ya Kilimo ambalo kwa sasa ni sehemu
ndogo tu inayotumika na jengo la Kilimo ambalo kwa sasa linatumika
kama ghala.
Alisema
idadi ya mifugo inayochinjwa katika machinjio hayo kwa sasa ni ng’ombe 550
hadi 600 kwa siku za kawaida na siku za sikukuu ni ng’ombe 1,000 hadi 1,500.
“Halmashauri yetu ya Ilala hukusanya zaidi ya sh. milioni
118 kwa mwezi wakati Serikali Kuu hukusanya milioni 117 kila
mwezi,” alisema Meshaki.
No comments:
Post a Comment