WAZAZI wametakiwa kutokuwaficha nyumbani watoto wenye ulemavu bali kuwatafutia msaada wa kuwawezesha kuonesha vipaji vyao pamoja kutimiza ndoto zao katika maisha kama ilivyo kwa watoto wengine wasiokuwa na ulemavu.
Wito huo ulitolewa juzi na mwanachama Mkongwe wa Chama cha Wanawake Wakristo (YWCA), Doroth Steven, katika mahafali ya wanafunzi wa chekechea katika kituo cha Furaha ambacho kiko chini ya YWCA ambapo watoto wenye ulemavu waliweza kuonesha vipaji vyao mbalimbali ikiwemo kuimba.
Alisema wazazi wangejua watoto hao walivyo na vipaji pamoja uhitaji wa haki zao kama ilivyo kwa watoto wengine, wasingewafungia ndani.
"Wazazi mnaozaa watoto wenye ulemavu msiwafungie ndani, watoto hawa wana vipaji sana. Mmeshuhudia jinsi walivyotuimbia hapa leo na kuonesha vipaji vyao vingine...kwahiyo ukimpeleka shule anajichanganya na wenzake na kuinua vipaji vyake pamoja na kutimiza ndoto zao," alisema Doroth.
Hata hivyo aliiomba Serikali kwa kushirikiana na wadau kuongeza vituo vingi zaidi ili kuwasiadia watoto wengi walio na ulemavu pamoja na kusaidia katika kuhamasisha jamii kutokuwaficha ndani watoto wenye
ulemavu kutokana na mila na desturi potofu.

Katibu wa tawi la YWCA Dar es Salaam, Monica Kimaro alisema katika mahafali hayo jumla ya watoto 30 wamehitimu, huku watoto 15 wenye ulemavu mbalimbali wanaendelea kusoma.
Akizungumzia kuhusu mikakati ya kukiendeleza kituo hicho alisema mpaka sasa ipo mikakati ya kufungua matawi ya kituo hicho nchi nzima ili kuwasaidia watoto wenye ulemavu katika maeneo mbalimbali nchini.
“Tuna fund rising ambayo ni ya dunia nzima na mwezi uliopita tulikuwa nchini Nertherland ambao wameahidi kutusaidia kujenga kituo cha watoto wenye ulemavu wa akili na viungo ambacho kitachukua watoto takriban
200 na tumeshanunua shamba eneo la kiluvya ambapo kutajengwa kituo hicho” alisema.
Naye Salome Lyimo, ambaye ana mtoto mwenye ulemavu alisema tangu amempeleka katika kituo hicho amekuwa mabadiliko kwani kwa sasa anaweza kuongea na kusoma tofauti na ilivyokuwa hapo awali.
No comments:
Post a Comment