HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

December 02, 2019

Msigwa atoa utetezi wake

Viongozi wa Chadema wakiwa katika kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam leo.


Na Janeth Jovin


MBUNGE wa Iringa, Peter Msigwa (Chadema) ameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa maadili ya Uchaguzi hayaruhusu kutolewa kwa hotuba za viashiria vya chuki na uvunjifu wa amani wakati wa Kampeni za Uchaguzi.

Msigwa ambaye anayekabiliwa na kesi ya uchochezi pamoja na vigogo wengine nane wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), alieleza hayo jana katika Mahakamani hapo wakati akitoa utetezi wake mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Thomas Simba.

Akihojiwa na wakili wa serikali Mkuu Faraja Nchimbi, Msigwa alidài kuwa maadili hayo pia yanazuia watu kuingia katika vituo vya kupigia kura wakiwa na siraha.

Msigwa alidai, aliudhuria mkutano wa kufunga Kampeni ya uchaguzi wa marudio jimbo la Kinondoni Februari 16 mwaka jana na kwamba baadhi ya viongozi na wabunge waliotoa hotuba hawapo mahakamani.

"Mimi binafsi nilihutubia  wananchi, sikumbuki kama Mdee alihutubia,  Mbowe pia alihutubia" alidai Msingwa.

Mshtakiwa huyo alidai washtakiwa wenziwe ni miongoni mwa Viongozi wa chadema walioudhulia mkutano huo na kuna baadhi ya wabunge waliohutubia 
katika mkutano huo lakini hawapo mahakamani.

Alitaja baadhi ya wabunge hao ni Frank Mwakajoka, Ernest Silinde, Said Kubenea, Mwita Waitara na John Heche.

Alidai,anapokuwa katika mkutano wa hadhara  lengo hadhira imuelewe,hivyo lazima azungumze lugha wanayoielewa kwani wanahutubia watu wa biwango tofauti vya uwelewa.

Katika hatua nyingine alidai, hajawahi kufanya kazi Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) ama ofisi ya Msimamizi wa Uchaguzi na kwamba Uchaguzi Mkuu husimamiwa na tume hiyo.

Washitakiwa wengine ni   katika kesi hiyo ni Mbunge wa Iringa mjini, Peter Msigwa, Naibu Katibu Mkuu Taifa, Zanzibar, Salum Mwalimu,  Mbunge wa Kibamba, John Mnyika,  Katibu Mkuu Taifa, Vicent Mashinji , mbunge wa Bunda Ester Bulaya na Mbunge wa Kawe  Halima Mdee.
Wengine ni Mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche,
Dokta Vicent Mashinji ambaye ni ,Katibu Mkuu taifà wa chama hicho na Ester Matiko.

Washitakiwa wanakabiliwa na mashitaka 13 likiwemo la kula njama, ambapo wote wanadaiwa kuwa, Februari 1 na 16, mwaka jana, Dar es Salaam walikuĺa njama ya kutenda kosa la kufanya mkusanyiko usio halali na kukiuka tamko kutawanyika.

No comments:

Post a Comment

Pages