HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

December 02, 2019

OPEN KITCHEN YAWAKUMBUKA WAJANE WENYE VVU

Katibu wa kikundi cha wajane wanaoishi na VVU, Carolline Damiani, akizungumza na mwandishi wa habari wakati ya hafla ya Chakula cha jioni ya kukichangia kikundi hicho.

 
Na Irene Mark

KIKUNDI cha Wajane 15 wajasiriamali wanaoishi na Virusi Vya Ukimwi kutoka wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam wamekabidhiwa zaidi ya Sh. Milioni 11 kutoka kwa kampuni ya Open Kitchen.

Makabidhiano ya fedha hizo yalifanyika jana siku ya Ukimwi Duniani wakati wa chakula cha jioni kilichoandaliwa na kampuni hiyo chini ya mradi wa 'Amka Twende'.

Akizungumza na waandishi wa habari walioshiriki hafla hiyo, Mkurugenzi wa Open Kitchen, Upendo Mwalongo alisema lengo ni kuwakutanisha na wajasiriamali wakubwa ili kubadilishana mawazo na uzoefu.

Mwalongo alisema fedha hizo ni sehemu ya mauzo ya tiketi za hafla hiyo iliyowalutanisha wajasiriamali wa vitu tofauti huku akisisitiza kwamba wana kikundi hicho watapata cha kujifunza, mbinu za kujitangaza na ujasiri wa kuzungumza kwenye had hata ya watu.

"Lengo langu ni kuhakikisha hawa ninaoanza nao wanakua ndio maana nimeenda Temeke na niliposikia changamoto zao niliguswa sana nikaamua hii fundraising ya leo ni kwaajili yao," alisema Mwalongo.

Katibu wa kikundi hicho, Caroline Damiani alisema changamoto kubwa wanayokutana nayo ni unyanyapaa hali iliyowalazimu kubadili aina ya biashara.

"Tulikuwa tunapika vyakula lakini tumeshindwa, tunakosa wateja sababu tunaishi na VVU wanasahau kwamba huu ugonjwa hauambulizwi kwa chakula. 

"...Sasa hivi tunafanya shughuli za mikono kutengeneza nyungo, vikapu, mikeka na ufumaji ndio tunauza tunategemea kuishi na familia zetu kwa biashara hii," alisema Damiani.

Mkurugenzi wa mgahawa wa On point, Justine Mabuki alisema hafla hiyo itakuwa chachu kwa kikundi hicho na wajasiriamali wengine kuongeza juhudi kwenye biashara zao.

No comments:

Post a Comment

Pages