HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

December 12, 2019

TAMASHA LA MOYO WA IBADA KUTIKISA DESEMBA 13, 2019

Mwandaaji wa tamasha la Moyo wa Ibada, Paul Mwangosi, akizungumza na waandishi wa habari kuelekea tamasha hilo linalotarajiwa kufanyika kesho Desemba 13, 2019 katika viwanja vya Tanganyika Parkers jijini Dar es Salaam.
 Mwimbaji wa nyimbo za injili kutoka Kenya, Sarah Mwangi ‘Sarah K’, akizumgumza na waandishi wa habari kuhusu tamasha la Moyo wa Ibada litakalofanyika Desemba 13, 2019 katika viwanja vya Tanganyika Parkers jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Jeremi Kitiku na Mwandaaji wa tamasha hilo, Paul Mwangosi.
 Mwimbaji wa nyimbo za injili kutoka Kenya, Sarah Mwangi ‘Sarah K’, akiimba moja ya nyimbo zake wakati wa mkutano na waandishi wa habari jana kuelekea tamasha la Moyo wa Ibada litakalofanyika Desemba 13, 2019 katika viwanja vya Tanganyika Parkers jijini Dar es Salaam. (Picha na Francis Dande).
Na Mwandishi Wetu 

MSIMU wa pili wa Tamasha la Mkesha wa Usiku wa Moyo wa Ibada utaunguruma kesho katika Viwanja vya Tanganyika Packers Kawe jijini Dar es Salaam. 

Tamasha hilo linaandaliwa na huduma ya Moyo wa Ibada chini ya Mwimbaji wa nyimbo za Injili Paul Mwangosi. 

Lengo Kuu ni kuwakutanisha watanzania kurudisha shukrani kwa Mwenyezi Mungu na kusema asante kwa ulinzi wa mwaka mzima  sabamba na kuliombea Taifa katika nyanja mbalimbali.

Akizungumza kuelekea Tamasha hilo Paul Mwangosi amesema ni mkesha wa Ibada ya kumsifu , kuabudu na kumshukuru Mungu. 

"Tutakutana hapa kwa ajili ya kumshukuru Mungu kwa kutulinda mwaka mzima, tutaimba na kusifu sambamba na kupata neno la uzima lakini pia tutapata nafasi ya kusema neno kwa ajili ya nchi yetu. 

"Natamani kila mmoja awe sehemu ya tamasha hili na sehemu ya ibada hii kama ambavyo ndugu zetu kutoka kenya wamekuja kujumuika nasi ."amesema Mwangosi. 

"Mwenyezi Mungu alituumba ili tumuabudu  kwani kumuimbia na kumsifu hata wanyama na mimea inafanya hivyo, ndio maana hatuchukulii kawaida kwa sababu imepangwa. 

"Katika kumsifu, kumuimbia na kumuabudu Mungu kuna mambo mengi hufunguka kwenye maisha yetu, huu ni wajibu wetu kusema asante kwa kutuwezesha kuumaliza mwaka Salama."amesema Sarah Mwangi mwimbaji wa nyimbo za Injili kutoka Kenya. 

Tamasha hilo linatarajiwa kuanza majira ya saa 3 usiku hadi alfajiri ya kuamkia Desemba 14. Wahudumu wanaotarajiwa kuhudumu ni pamoja na Mwandaaji Paul Mwanaidi,  Sarah Mwangi (Kenya) na Boaz Danken.

No comments:

Post a Comment

Pages