Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James (kulia), na Naibu
na Kaimu Balozi wa Japan nchini Tanzania, Bw.
Katsutoshi Takeda, wakisaini mkataba wa Msaada wa Sh. 4.2 kwa ajili ya kufufua
Shirika la Uvuvi Tanzania (TAFICO), hafla iliyofanyika katika ukumbi wa Wizara
ya Fedha na Mipango, Jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James (kulia), na Naibu
na Kaimu Balozi wa Japan nchini Tanzania, Bw.
Katsutoshi Takeda, wakibadilishana mkataba wa Msaada wa Sh. 4.2 kwa ajili ya
kufufua Shirika la Uvuvi Tanzania (TAFICO) ambapo TAFICO itaweza itaweza kuwa
na Meli ya Uvuvi, hafla hiyo iliyofanyika katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na
Mipango, Jijini Dar es Salaam
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James (kulia), na Naibu
na Kaimu Balozi wa Japan nchini Tanzania, Bw.
Katsutoshi Takeda, wakiwa wamenyenyua Mkataba wa Msaada wa Sh. 4.2 kwa ajili ya
kufufua Shirika la Uvuvi Tanzania (TAFICO), hafla iliyofanyika katika ukumbi wa
Wizara ya Fedha na Mipango, Jijini Dar es Salaam.
Na Peter Haule, WFM, Dar es Salaam
Tanzania imepokea msaada wa Yen za Japan milioni 200
sawa na Shilingi Bilioni 4.2 kutoka Serikali ya Japan kwa ajili ya kufufua
Shirika la Uvuvi Tanzania (TAFICO)
Mkataba wa msaada huo umesainiwa na Katibu Mkuu wa
Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James, kwa niaba ya Serikali ya Tanzania
na Naibu na Kaimu Balozi wa Japan,
Bw. Katsutoshi Takeda, kwa niaba ya
Serikali ya Japan.
Katibu Mkuu, Bw. Doto James, alisema kuwa msaada huo
utatumika kununua Meli ya Uvuvi yenye vifaa vya kisasa, mashine ya kutengeneza barafu, ghala
la baridi la kuhifadhia samaki, Vifaa mbalimbali vya kuvulia samaki na vya
karakana, gari lenye mitambo maalum ya barafu na Gari kwa ajili ya kusambazia
samaki.
Alisema
kuwa utekelezaji wa Mradi huu utachangia kwa kiasi
kikubwa katika kufikia malengo ya Mpango wa Maendeleo wa Miaka Mitano Awamu ya
Pili (FYDP II), ambayo pamoja na mengine unalenga kuboresha Sekta ya Uvuvi na
hatimaye kuvutia Watanzania zaidi kujihusisha katika Sekta ya Uvuvi kama
shughuli kuu ya kujipatia kipato.
“Mradi huu utaongeza uuzaji wa samaki nje ya nchi,
kuongeza uhakika wa chakula nchini, na pia utaboresha usindikaji wa samaki,
kuongeza thamani na masoko na kupunguza upotevu wa mazao ya samaki baada ya kuvua”,
alieleza Bw. James.
Alisema kuwa Kiwango
cha ukuaji kwa shughuli ndogo za kiuchumi za uvuvi kilifikia asilimia 9.2 mwaka
2018 ikilinganishwa na ukuaji wa asilimia 8.4 mwaka 2017 ambapo kiwango kikubwa
cha ukuaji kilitokana na utunzaji mzuri wa mazalia ya samaki yakiwemo mabwawa
ya watu binafsi sambamba na kuongezeka kwa mahitaji katika soko la ndani na
nje.
Bw. James alisema kuwa, shughuli za uvuvi zilichangia asilimia 1.7
katika Pato la Taifa mwaka 2018, ambayo inadhihirisha umuhimu wa uvuvi katika
uchumi, hivyo msaada uliotolewa utachangia jitihada za Serikali katika kufikia
Dira ya Maendeleo ya mwaka 2025, Malengo Endelevu ya mwaka 2030 na Agenda ya
Maendeleo ya Afrika ya mwaka 2063.
Alisema kuwa
Serikali ya Japan imekuwa ikiisaidia Tanzania kupitia misaada na mikopo nafuu
katika Sekta mbalimbali ikiwemo Kilimo, Miundombinu ya barabara, Maji, Nishati Utawala Bora na Uwajibikaji ambapo
mpaka sasa Jumla ya Sh. Trilioni 1. 3 zimetolewa na Serikali hiyo tangu mwaka 2012.
Misaada na mikopo
hiyo inadhihirisha kuwa kuna uhusiano mzuri wa kirafiki kati ya Tanzania na
Serikali ya Japan, hivyo matumaini ni kuwa urafiki huo utaendelea kuimarishwa
na Serikali zote mbili kwa ajili ya maendeleo ya nchi hizo.
Kwa upande wake Naibu na
Kaimu Balozi wa Japan, Bw. Katsutoshi
Takeda, kwa niaba ya Serikali ya Japan
amesema nchi yake itaendelea kuisaidia Tanzania kutokana na ushirikiano mzuri
kati ya nchi hizo mbili lakini pia kuchangia jitihada za Serikali ya Tanzania
katika kukuza uchumi na kuondoa umasikini wa wananchi wake.
Naye Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi,
Dkt. Rashid Tamahtamah ameishukuru Serikali ya Japan kwa msaada huo
utakaosaidia kufufua Shirika hilo la Uvuvi.
Alisema kuwa Serikali itapeleka mswaada Bungeni
mwezi Januari mwakani, ili kuliwezesha TAFICO kuanza kazi zake rasmi na kwa
kishindo ili Shirika hilo liweze kuchangia katika uchumi wa Taifa kwa kiwango
kikubwa.
Alisema kuwa pamoja na msaada huo, Serikali
imechukua hatua za kuchambua mali zilizokuwa zikimilikiwa kinyemela na baadhi
ya taasisi na watu ambapo mpaka sasa mali zenye thamani ya zaidi shilingi
bilioni 118 zimerejeshwa Serikalini na kazi ya kurejesha mali nyingine
zinaendelea kwa kushirikiana na Msajili wa Hazina.
No comments:
Post a Comment