HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

December 14, 2019

UFARANSA YAONGEZA UFADHILI KWA WANAFUNZI WA TANZANIA

 
 Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, William Ole Nasha, akiongozana na balozi wa Ufaransa nchini Tanzania, Frederic Clavier, wakati akiwasili katika kongamano la vyuo vikuu vya Tanzania na Ufaransa lililofanyika leo Desemba 14, 2019 jijini Dar es Salaam ambapo zaidi wanafunzi 900 wamehudhuria kongamano hilo.

Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania, Frederic Clavier, akizungumza katika kongamano la vyuo vikuu vya Tanzania na Ufaransa lililofanyika leo Desemba 14, 2019 jijini Dar es Salaam ambapo zaidi wanafunzi 900 wamehudhuria kongamano hilo.

Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania, Frederic Clavier, akizungumza katika kongamano la vyuo vikuu vya Tanzania na Ufaransa lililofanyika leo Desemba 14, 2019 jijini Dar es Salaam ambapo zaidi wanafunzi 900 wamehudhuria kongamano hilo.

Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, William Ole Nasha, akimpongeza Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania, Frederic Clavier, baada ya kutoa hotuba yake.

Baadhi ya washiriki wa kongamano hilo.

Mwakilishi wa Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, akitoa hotuba yake.

Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, William Ole Nasha, akifungua rasmi kongamano la vyuo vikuu vya Tanzania na Ufaransa lililofanyika leo Desemba 14, 2019 jijini Dar es Salaam.

Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania, Frederic Clavier, akimpongeza Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, William Ole Nasha, baada ya kutoa hotuba yake.

Rais wa wanafunzi waliosoma Ufaransa, Manday Israel, akizungumza katika kongamano hilo.

Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, William Ole Nasha, akimsikiliza balozi wa Ufaransa nchini Tanzania, Frederic Clavier.

Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, William Ole Nasha, akimsikiliza balozi wa Ufaransa nchini Tanzania, Frederic Clavier. 

 Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, William Ole Nasha, akiagana na balozi wa Ufaransa nchini Tanzania, Frederic Clavier.

Baadhi ya wanafunzi wakipata maelezo ya namna ya kujiunga na vyuo vikuu vya ndani na nje ya nchi.





Na Mwandishi Wetu

SERIKALI ya Ufaransa imeongeza idadi ya ufadhili wa kuwasomesha wanafunzi wanaotaka kusoma nchini humo katika fani mbalimbali lengo likiwa ni kukuza ushirikiano na uhusiano wa pande hizo mbili katika Sekta ya Elimu.

Kauli hiyo imetolewa leo Desemba 14, 2019 na Naibu Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia, Willian Ole Nasha, wakati wa mkutano uliovikutanisha Vyuo Vikuu 10 kutoka Tanzania na vingine 10 kutoka nchini Ufaransa yakiwemo makampuni makubwa zaidi ya 40 ya nchi hiyo.


Amesema serikali ya nchi hiyo kupitia balozi wake aliyepo nchini walikubali kuongeza udhamini wa kuwasomesha wanafunzi 50 kutoka 30 wanaowapatia ufadhili kila mwaka wa kuwasomesha nchini humo

“Ufaransa imekuwa ikisaidia sana nchi yetu katika Sekta ya Elimu na hutoa ufadhili kwa wanafunzi kila mwaka ambapo hiyo ni tofauti na ufadhili unaotolewa na makampuni”amesema Ole Nasha

Ole Nasha amesema mkutano huo pia uliwakutanisha pamoja zaidi ya wanafunzi 900 kutoka vyuo mbalimbali nchini lengo likiwa ni kufanya mijadala kuhusu masuala ya Elimu,Ajira na Utafiti ambapo wanafunzi wanapata fursa ya kupata taarifa juu ya kozi zinazotolewa ufaransa na kupata fursa ya kupata udhamini wa kusomeshwa.

Amesema hata hivyo kupitia makampuni hayo wanaweza kupata ajira kutokana na aina kozi ambazo wanafunzi hao wamesomea hivyo kuwa ni mkutano muhimu kwa Tanzania.

“Marafiki huongea lugha moja kama wao wanavyotaka sisi tuongee kifaransa na mimi nimemuomba balozi ahakikishe kuwa na wao wanafundisha kifaransa”amesema Ole Nasha.

Ameongeza kuwa elimu inayotolewa kwa sasa nchini ni elimu inayojenga ubunifu na kujiamini kwani duniani kote sekta binafsi ndio inayoajiri watu na serikali huajiri watu wachache.

No comments:

Post a Comment

Pages