WANAHARAKATI
mbalimbali wameomba elimu kuhusu masuala ya ukatili wa jinsia iendelee
kutolewa kuanzia ngazi ya chini mpaka ya juu, ili kuweza kuvitokomeza
vitendo hivyo.
Pia wanaharakati hao wameomba kuanzishwa kwa madawati ya kijinsia kuanzia katika serikali za mitaa.
Hayo
waliyabainisha mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam katika muendelezo
wa semina za Jinsia na Maendeleo (GDSS) ambazo huratibiwa na Mtandao wa
Jinsia Tanzania (TGNP Mtandao) na hufanyika kila Jumatano.
Mwanaharakati
Anna Kikwa akizungumza kwenye semina hiyo iliyobeba ujumbe ‘Nafasi ya
jamii katika vita ya kutokomeza ukatili wa kijinsia’, alisema elimu
inahitajika kwa kushirikana na wadau wengine ili kuleta nguvu ya pamoja.
“Ili
tufanikiwe katika kupinga ukatili wa kijinsia tunapaswa kufanya kwa
pamoja, jamii, wadau ili kutokomeza matukio ya ukatili,” alisema Kikwa.
Naye
Mwanaharakati Janeth Mawinza alisema kuanzishwa kwa madawati ya
kijinsia kuanzia ngazi ya mitaa itasaidia taarifa kutolewa bila vikwazo.
Alisema
baadhi ya wanakumbwa na ukatili huo wanapatwa na woga wa kufika polisi
na kwamba unazishwaji wa madawti mtaani kutaongeza takwimu za taarifa
zinazotokea kwenye jamii.
“Kuwepo
na motisha wa wanaharakati ambao wamekuwa wakipambana na hata
kuhatarisha maisha yao, binafsi nilifikia kuhatarisha maisha wakati
nikifuatilia kesi fulani kuhusu ukatili wa kijinsia,“ alisema Mawinza.
No comments:
Post a Comment