HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

December 07, 2019

Watashauri upatikanaji mbegu asili uongezwe

 Baada ya washiriki wa mkutano wa kimataifa wa kilimo hai.
 Baada ya washiriki wa mkutano wa kimataifa wa kilimo hai uliofanyika kwa siku mbili jijini Dodoma hivi karibuni.
Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano kutoka Shirika la TOAM, Constantine Akitanda akimueleza jambo Waziri wa Kilimo, Chakula na Mifugo Japhet Hasunga aliyekuwa mgeni rasmi wakati wa ufunguzi wa mkutano wa kimataifa wa kilimo hai uliofanyika jijini Dodoma hivi karibuni.
Waziri wa Kilimo, Chakula na Mifugo, Japhet Hasunga, akisikiliza maelezo ya wajasiriamali wa kilimo hai waliohudhuria mkutano wa kimataifa wa kilimo hai na kuonesha bidhaa na mazao ya asili.

Na Irene Mark

UPATIKANAJI wa mbegu asili kwa ajili ya kilimo hai ni changamoto hivyo Serikali imetakiwa kuibua mjadala wa kuhamasisha mabadiliko ya sheria ili kurahisisha usamabazaji wa mbegu hizo.

Hayo yalisemwa na wadau wa kilimohai hivi karibuni jijini Dodoma wakati wa mkutano wa kimataifa na maonesho ya sekta hiyo.

Mkutano huo uliandaliwa na Shirika la Kuendeleza Kilimo Hai (TOAM), likishirikiana na Shirika la Chakula la Umoja wa Mataifa (FAO) na Ubalozi wa Ufaransa.

Kwa nyakati tofauti wadau hao walisema wanakabiliwa na changamoto kubwa ya upatikanaji wa mbegu asili ukilinganisha na mbegu za kisasa ambazo si rafiki kwenye kilimo hai.

Mkulima na mwakilishi kutoka Kampuni ya Biore Textile Exchange, Marco Paulo, alisema kilimo hai kinatakiwa kutangazwa na mbegu zake kuwa rahisi kupatikana ili kukabiliana na kilimo cha kisasa chenye mjadala mkubwa barani Afrika kwa sababu ya athari zake kiafya.

Alisema kilimo cha kisasa kinasababisha umiliki wa mbegu, kuongezeka kwa viuatilifu na usugu wa wadudu waharibifu shambani hivyo ni hatari kwa mazingira na afya za binaadamu.

"Naishauri serikali iweke mkakati wa kisheria kabisa wa kuhakikisha mbegu za asili zinapatikana kwa wingi na kuwafikia wakulima huko vijijini kutokana na umuhimu wa kiafya wa kupata mazao asili yanayotokana na kilimo hai.

"Athari za matumizi ya mbegu za kisasa zipo kijamii, kiafya, kiuchumi, kimazingira na asilimia 95 ya mbegu kumilikiwa na kampuni moja.

"Mbegu hizi hazina faida kiuchumi kwa wakulima kwa kuwa huwezi kuzitunza kila mwaka mkulima anatakiwa kununua mbegu... hii ni hasara," alisema Paulo.

Mwakilishi wa FAO, Mponda Malozo alisema ni vema katika matumizi ya kilimo kukawekwa kipaumbele cha afya na lishe.

Aliwashauri watunga sera kuangalia namna sahihi ya kusimamia kilimo hai na wakulima nao wakajipanga kuongeza uzalishaji wa chakula usio na athari kwa afya na mazingira.

Mwakilishi wa Kampuni ya Bio Vision, Nancy Rapando alisema, ipo haja ya kujenga mifumo ya vyakula kwa kupima kilimo hai ili kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.

No comments:

Post a Comment

Pages