HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

February 11, 2020

BALOZI KANALI IBUGE AKUTANA,KUFANYA MAZUNGUMZO NA SEKRETARIETI YA SADC

 Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Kanali Wilbert A. Ibuge akiongea na Mkurugenzi wa Rasilimali watu na Utawala wa SADC, Bibi. Bodo Tanrely Radaody Ravarosy leo katika Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Kanali Wilbert A. Ibuge akiwa katika picha ya pamoja na Sekretarieti ya SADC pamoja na watumishi wa Wizara.
Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Kanali Wilbert A. Ibuge akiagana na Mkurugenzi wa Rasilimali watu na Utawala wa SADC, Bibi. Bodo Tanrely Radaody Ravarosy.

 Na Mwandishi Wetu

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Kanali Wilbert A. Ibuge amekutana na kufanya mazungumzo na Sekretarieti ya Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC). 

 

Pamoja na mambo mengine, Katibu Mkuu alipokea taarifa ya ziara ya Sekretarieti ya SADC na kuwahakikishia ushirikiano wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hususan Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki katika kufanikisha mikutano yote ya SADC kipindi cha
Uenyekiti wa Tanzania.


Ujumbe wa Sekretarieti ya SADC unaongozwa na Mkurugenzi wa Rasilimali watu na Utawala wa SADC, Bibi. Bodo Tanrely Radaody Ravarosy ambao wapo nchini kwa ajili ya maandalizi ya mkutano wa Mawaziri wa Mambo ya
Nje wa SADC unaotarajiwa kufanyika tarehe 10 - 11 Machi, 2020, Jijini Dar es Salaam ambapo pamoja na mambo mengine, ujumbe huo ulipata fursa ya kukutana na Katibu Mkuu Balozi Ibuge na kumpa taarifa ya maandalizi ya
mkutano huo.


Mwezi Augosti, 2019 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Joseph Pombe Magufuli alipokea rasmi Uenyekiti wa SADC katika Mkutano wa Wakuu wa Nchi wanachama.


Aidha, hatua hiyo ilifuatiwa na mikutano mbalimbali ya kisekta iliyofanyika na inayoendelea kufanyika hapa nchini kwa kipindi cha kuanzia mwezi Septemba 2019 hadi Agosti, 2020 ambapo hadi sasa imeshafanyika
mikutano mitatu ya kisekta.
 

Mikutano hiyo ni pamoja na Mkutano wa Mawaziri wa SADC wenye dhamana ya masuala ya Tehama, Habari, Uchukuzi na hali ya Hewa, Mkutano wa Pamoja wa Mawaziri wa Sekta ya Afya na VVU na UKIMWI pamoja na mkutano wa pamoja wa Mawaziri wa Mazingira, Maliasili na Utalii.

No comments:

Post a Comment

Pages