Wanachama wa Kundi la Simba Jamii Tanzania (SJT), wakitoa msaada wa vitu
mbalimbali kwa Kituo cha Watoto Yatima cha Mindu Bwawani Morogoro leo.
Na Mwandishi Wetu
KUNDI maarufu la Simba SC Jamii Tanzania (SJT) leo limetoa misaada mbalimbali yenye thamani ya Sh.Mil. 13 kwa kituo cha watoto yatima cha Mindu Bwawani kilichopo eneo la Mindu, Morogoro.
Kwa mujibu wa Katibu wa Kamati ya Matukio wa Simba Jamii, Magambo Matango alisema wameonesha kuguswa na mazingira wanayolelewa watoto hao yatima hivyo wataendelea kusaidia kila wakipata fedha.
Matango alisema misaada waliyoiwasilisha katika kituo hicho ni pamoja na madaftari, kalamu na vifaa vingine vingi ambavyo vitawasaidia watoto hao.
Magambo alisema wametekeleza matakwa hayo kwa malengo ya kuikumbuka jamii ya watanzania wa kila kona, kwa sababu jamii ni sehemu ya maisha yao ya kila siku.
Aidha Magambo alisema baada ya kutoa msaada huo kwa kituo cha Mindu, leo kundi hilo linatarajia kukabidhi baiskeli za walemavu ikiwa ni sehemu ya kuendeleza misaada hiyo kwa jamii.
“Kundi letu limejikita zaidi kwenye kusaidia jamii yenye uhitaji, tumeanzia Mindu, tunaendelea na maeneo mengine kama ya walemavu ambao nao ni sehemu ya wenye uhitaji, tunawaomba wadau wengine kuiga mfano kama tuliouanzisha ili tuisaidie jamii yetu,” alisema Magambo.

Jamii yetu Simba yetu
ReplyDelete