HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

February 26, 2020

KIPATO CHANZO CHA KUONDOKANA NA UKATILI WA KIJINSIA

 Mwakilishi wa Katibu Mkuu Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii Bi. Imelda Kamugisha akieleza namna Serikali inavyowawezesha wananchi kuondokana na vitendo vya ukatili wakati msafara wa kijinsia wa kutokomeza ukatili wa Kijinsia.
  Msanii Shetta na G nako wakitumbuiza eneo la Mlowa Mbozi mkoani Songwe wakati msafara wa kijinsia wa kutokomeza ukatili wa kijinsia ulipokuwa mkoani hapo.
 

Na Mwandishi Wetu, Songwe

Uwepo wa kipato katika familia hasa mwanamke akiwezeshwa kiuchumi inapunguza kuwepo kwa vitendo vya ukatili katika jamii zetu.

Hayo yamebainishwa Mlowa Mkoani Songwe na Mwakilishi wa Katibu Mkuu Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii Bi. Imelda Kamugisha wakati msafara wa kijinsia wa kutokomeza ukatili wa kijinsia uliposimama Mkoani hapo.

Amesema kuwa Serikali katika kupambana na vitendo vya ukatili imeanzisha mpango mkakati wa kitaifa wa kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto uliozinduliwa mwaka 2017/2018 na utamalizika mwaka 2021/2022.

No comments:

Post a Comment

Pages