Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mhe. Juma Zuberi Homera akizungumza na
wananchi wa Wilaya Mpanda wakati wa uzinduzi wa Msafara wa kijinsia leo
mkoani humo.
Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mhe. Juma Zuberi Homera akiagana na Msanii Shetta mara baada ya kuzindua Msafara wa kijinsia wa kutokomeza ukatili leo mkoani Katavi.
Msanii wa Muziki wa kizazi kipya Nurdin Bilal maarufu Shetta akitumbuzia wanafunzi wakati wa uzinduzi wa Msafara wa kijinsia wa kutokomeza ukatili leo mkaoni Katavi.
Mwakilishi wa Katibu Mkuu Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii, Bi. Imelda Kamugisha, akieleza lengo la msafara wa kijinsia wa kutokomeza ukatili uliozinduliwa leo Mkoani Katavi.
Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mhe. Juma Zuberi Homera akiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, mkoa wa Katavi na wasanii mara baada ya kuzindua Msafara wa kijinsia leo mkoani humo. Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini WAMJW

Mkuu
wa Mkoa wa Katavi Mhe. Juma Zuberi Homera akipata maelezo kutoka kwa
Afisa Ustawi wa Jamii, Caren Mitta, kuhusu utaoji wa huduma za Ustawi wa
jamii katika Msafara huo uliozinduliwa leo mkoani Katavi.
Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mhe. Juma Zuberi Homera akiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, mkoa wa Katavi na wasanii mara baada ya kuzindua Msafara wa kijinsia leo mkoani humo. Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini WAMJW
Na Mwandishi Wetu, Katavi
Msafara
wa kijinsia unaolenga kutokomeza vitendo vya kikatili kuelelekea Siku
ya Wanawake Duniani umezinduliwa rasmi mkoani Katavi.
Akizungumza
wakati akizindua Msafara huo Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mhe. Juma Zuberi
Homera amesema kuwa vitendo vya kikatili vimekuwa vikishamiri kila siku
katika jamii zetu hivyo vinatakiwa kupatiwa mbinu ya kupambana navyo.
Ameongeza
kuwa Serikali haiwezi kuvumilia kuona wanawake na watoto wanafanyiwa
vitendo vya kikatili hivyo itahakikisha inazishugulikia kesi zote za
vitendo vya ukatili.
"Sheria ifuate mkondo hata mimi naweza kutelekezwa na hata mimi nikitelekeza nikamatwe tu" alisema
Mhe.
Homera amesisitiza vyombo vya Sheria na Taasisi zisizo za Kiserikali
kushirikiana pamoja katika kuhakikisha wanapata mbinu stahiki
itakayosaidia kuondokana na vitendo vya ukatili.
Akizumgumza
kwa niaba ya Katibu Mkuu Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii, Afisa
Maendeleo ya Jamii Mkuu Bi. Imelda Kamugisha amesema lengo la msafara
huo ni kutoa elimu kwa wananchi kuhusu madhara ya vitendo vya ukatili na
namna ya kupambana na vitendo hivyo kuelekea maadhimisho ya Siku ya
wanawake Duniani.
"Msafara
huu umelenga kutoa elimu kwa kuwafuata wananchi katika maeneo yao ili
kuendeleza jitihada za Serikali na wadau katika kuhakikisha tunaondokana
na vitendo vya kikatili" alisema
Naye
Nurdin Bilal Maarufu Shetta amesema wasanii wameungana na Serikali
katika kusambaza elimu ya kupambana na vitendo vya ukatili ili kuwezesha
kuondokana na vitendo hivyo kwa asilimia 25 ifikapo mwaka 2025.
"Tuko tayari na tumeamua wasanii kuingia katika haya mapambano muhimu ya kitaifa dhidi ya vitendo vya kikatili" alisema.
No comments:
Post a Comment