Wahasibu na Wakaguzi wa Ndani wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania
(TAA), leo wakiwa kwenye mafunzo ya uandaaji na uwakilishwaji wa vitabu
vya Hesabu za fedha kwa kuzingatia viwango vya Kimataifa vya Uhasibu kwa
Taasisi za serikali (IPSAS accrual), yanayofanyika kwa siku tano kwenye
ukumbi wa mikutano wa Jengo la Pili la Abiria la Kiwanja cha Ndege cha
Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA_TB2).
Kaimu Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu wa Mamlaka ya
Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Renatus Msangira, akifungua mafunzo ya uandaaji
na uwakilishwaji wa vitabu vya Hesabu za fedha kwa kuzingatia viwango vya
Kimataifa vya Uhasibu kwa Taasisi za serikali (IPSAS accrual), yaliyoanza
leo kwenye ukumbi wa mikutano wa Jengo la Pili la Abiria la Kiwanja cha
Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA_TB2), kwa kushirikisha
Wahasibu na Wakaguzi wa Ndani.
Wahasibu na Wakaguzi wa Ndani wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania
(TAA), wakimsikiliza kwa makini aliyekuwa Kaimu Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali
Watu, Renatus Msangira akifungua mafunzo ya uandaaji na uwakilishwaji wa
vitabu vya Hesabu za fedha kwa kuzingatia viwango vya Kimataifa vya
Uhasibu kwa Taasisi za serikali (IPSAS accrual), yaliyoanza leo kwenye ukumbi
wa mikutano wa Jengo la Pili la Abiria la Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa
cha Julius Nyerere (JNIA_TB2).
Kaimu Mkurugenzi wa Fedha na Biashara wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege
Tanzania (TAA), CPA Josephine Kolola leo akizungumza na Wahasibu na
Wakaguzi wa Ndani wa Mamlaka hiyo, wanaoshiriki mafunzo ya uandaaji na
uwakilishwaji wa vitabu vya Hesabu za fedha kwa kuzingatia viwango vya
Kimataifa vya Uhasibu kwa Taasisi za serikali (IPSAS accrual), yanayofanyika
kwenye ukumbi wa mikutano wa Jengo la Pili la Abiria la Kiwanja cha Ndege
cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA_TB2). Mafunzo hayo yamefunguliwa na
aliyekuwa Kaimu Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu, Renatus Msanjira.
Mkurugenzi wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA),
Paul Rwegasha (kushoto) akizungumza na Kamishna Msaidizi wa Zimamoto na
Uokoaji (ACF) Bakari Mrisho (wa pili kushoto), aliyekuwa Kaimu Mkurugenzi
wa Utawala na Rasilimali Watu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania,
Renatus Msangira (kulia), na Meneja wa Utawala na Rasilimali Watu na
Mafunzo, Abdi Mkwizu.
Na Bahati Mollel, TAA
MAFUNZO ya uandaaji na
uwakilishwaji wa vitabu vya Hesabu za fedha kwa kuzingatia viwango vya
Kimataifa vya Uhasibu kwa Taasisi za serikali (IPSAS accrual), yameelezwa kuwa
yataondoa hoja za Wakaguzi wa ndani na nje.
Kaimu Mkurugenzi wa Fedha na
Biashara wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), CPA Josephine Kolola
amesema hayo wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo yaliyoanza leo kwenye Jengo la
Pili la Abiria la Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA-TB2)
kwa kushirikisha Wahasibu na Wakaguzi wa Ndani wa Mamlaka hiyo, ambapo yanashirikisha
washiriki 56 kutoka Viwanja vya ndege vya serikali vilivyopo Tanzania Bara.
“Pia ni matarajio yangu baada
ya mafunzo haya kutawezesha kupungua kwa kiasi kikubwa na hata kutokuwepo
kabisa kwa hoja za wakaguzi wa ndani na nje kutokana na uelewa utakapopatikana
kwa washiriki,” amesema CPA Kolola.
CPA Kolola amesema mafunzo
hayo pia yatashirikisha suala zima la maadili ya Uhasibu (Code of Conduct & Ethics for Professional accountants);
uzingatiaji wa miongozo mbalimbali ya kifedha kadiri inavyotolewa na serikali
(MoFP), hivyo kutoa taarifa za fedha zenye kuonesha uhalisia na mwelekeo wa
Mamlaka wenye tija kwa watumiaji wa taarifa hizo.
“Mafunzo haya yatawakumbusha
wahasibu wote wa Mamlaka dhamana waliyonayo katika masuala yote ya kifedha
hivyo kuwa makini katika kazi zao za kila siku kwa kuhakikisha umakini wa
kuingiza data za mapato, matumizi, madeni nk, hivyo kuepusha makosa kwenye
vitabu vya hesabu,” amesema CPA Kolola.
Awali akifungua mafunzo hayo
aliyekuwa Kaimu Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu wa TAA, Renatus
Msangira akimwakilisha Mkurugenzi Mkuu Mhandisi Mshauri Julius Ndyamukama, aliwataka
wahasibu na wakaguzi hao wa ndani kuhakikisha wanatunza siri za hesabu ya
taasisi hiyo, kwa kuwa ni kosa la kisheria kuzitoa kwa watu wasiohusika.
“Hesabu za taasisi au ofisi
yeyote ya Umma hazipaswi kusambazwa hovyo kwa watu wasiostahili hizo ni moja ya
siri na zinapaswa kutunzwa vyema, na hutolewa kwa kibali maalum endapo
itahitajika, lakini sio zaidi ya hapo” alisisitiza Msangira.
Pia amewataka washiriki hao
wapatao 56 kutoka viwanja mbalimbali vya ndege Tanzania Bara watumie fursa hiyo
kwa kuboresha utendaji wao wa kazi kwa kushirikiana vyema na Vitengo na Idara
zilizopo, ili kufanikisha lengo la Mamlaka la kuwa na hesabu bora.
Hatahivyo, aliwasisitizia
kufanya kazi kwa upendo, uadilifu na amani kwa kutojiwekea msongo wa mawazo
kwani wanaweza kuharibu kazi kutokana na akili kutokuwa sawa.
“Nina imani kubwa kwamba
mafunzo haya yatawaongezea kitu kikubwa sana katika kada zenu, hivyo mjaribu
kuzingatia kazi na kada zenu na msiingilie kazi zisizowahusu,” amesema.
Halikadhalika aliwasisitizia
kujiendeleza zaidi kitaaluma ili wapate CPA, ambayo itawaruhusu kukafanya kazi
kwa viwango vinavyohitajika kitaifa na kimataifa.
Mafunzo hayo ya siku tano
yanaendeshwa na Wataalam kutoka Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi Tanzania
(NBAA).
No comments:
Post a Comment