Mkuu wa mkoa wa Mara Adam Malima akimuonesha sehemu
ya maendeleo ya ujenzi wa jengo la hospitali ya Rufaa ya Kwangwa Musoma Naibu
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula alipofanya
ziara kukagua ujenzi wa hospitali hiyo jana, Jengo hilo linajengwa na Shirika
la Nyumba la Taifa (NHC). (Picha na Wizara ya Ardhi).
Na Munir Shemweta, WANMM MUSOMA
Naibu Waziri wa Ardhi
Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula amelitaka Shirika la Nyumba
la Tiafa (NHC) kuongeza kasi ya ujenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Kwangwa iliyopo
Musoma mkoa wa Mara ili kukamilika kwa muda uliopangwa.
Hospitali hiyo ya
Kwangwa ni ya ghorofa tano yenye shemu tatu (Wing A, B na C) na inarajiwa
kuanza kutoa Huduma kwa baadhi ya sehemu kati kati ya mwezi ujao
Dkt Mabula alitoa kauli
hiyo jana tarehe 25 Februari mjini Musoma mkoa wa Mara wakati wa ukaguzi
wa maendeleo ya ujenzi wa jengo hilo
unaofanywa na NHC akiwa katika ziara
yake ya siku moja.
Alisema, pamoja na NHC
kufanya vizuri katika ujenzi wa jengo la hospitali hiyo ukilinganisha na
wakandarasi waliotangulia lakini inapaswa kuongeza kasi ili likamilike katika
muda uliopangwa na kuanza kutoa huduma.
Kwa mujibu wa Mabula,
Hospitali ya Kwangwa itakayojulikana kwa jina la Mwl Nyerere Memorial Hospital ina
historia ndefu kwa kuwa pamoja na kuasisiwa na Rais wa Kwanza Mwalimu Julius
Nyerere lakini utekelezaji wake unakamilishwa na serikali ya awamu ya tano.
‘’Ni vyema NHC mkaongeza
bidii katika ujenzi wa hospitali hii ili ikamilike kwa haraka kwa kuwa
hospitali hii ina historia ndefu na Rais John Pombe Magufuli ameamua ujenzi huu
ukamilike kwa kutoa bilioni 15’’ alisema Mabula.
Katika kuhakikisha
ujenzi wa hospitali hiyo unakamilika kwa wakati, Naibu Waziri Mabula alimtaka
Mkurugenzi Mkuu wa NHC Dkt Maulid Banyani kusimamia kwa karibu maendeleo ya ujenzi
huo sambamba na kupatiwa ratiba ya mpango wa ujenzi na maendeleo yake kila
baada ya siku mbili kwa nia ya kufuatilia kwa karibu.
Hata hivyo, Mkurugenzi Mkuu
wa Shirika la Nyumba la Taifa Dkt Maulid Banyani alimuahakikishia Naibu Waziri Mabula
kuwa, ujenzi wa hospitali hiyo sasa utakamilika kwa wakati baada ya changamoto
kadhaa ikiwemo ya Mshauri Mwelekezi
kupatiwa ufumbuzi.
Kwa Upande wake Mkuu wa
mkoa wa Mara Adam Malima mbali na kuisifu NHC kwa kufanya mabadiliko makubwa ya
utekelezaji wa ujenzi wa mradi wa hospitali
ya Kwangwa alioueleza kuwa ilikwamwa kwa mara kadhaa.
‘’Toka Shirika la
Nyumba la Taifa lianze ujenzi wa hospitali hii mwezi Agosti mwaka jana kuna
mabadiliko makubwa ya kasi ya ujenzi
na tunataka mjenge kwa wakati na
viwango na Machi mwaka huu Huduma ya Mama na Mtoto ianze kutolewa ‘’ alisema
Malima.
Kwa mujibu wa Mkuu wa
Mkoa wa Mara, hospitali hiyo itatoa huduma kwa wananchi wa mikoa ya Kanda ya
ziwa pamoja na nchi jirani sambamba na kutumika kama sehemu ya utalii kutokana
na mazingira ya hospitali.
Historia ya Ujenzi wa
Hospitali ya Kwangwa iliyopo Musoma mkoa wa Mara inaanzia mwaka 1977 pale Rais
wa kwanza wa Mwl Nyerere alipotoa wazo la
kujengwa kwake lakini ujenzi huo umekuwa
ukikwama kwa nyakati tofauti hadi Rais John Pombe Magufuli alipotoa Shilingi
Bilioni 15 kwa lengo la kukamilishwa mradi huo ambapo sasa unatarajiwa
kukamilika mwaka huu.
No comments:
Post a Comment