Na Tiganya Vincent, TABORA
WAKAZI wa Kata ya Miswaki
wilayani Uyui wameiomba Serikali kuangalia uwezekano wa kuwachimbia Bwawa la
Maji ili kuwaondolea adha a matumizi ma maji ambayo sio salama na safi.
Kauli hiyo imetolewa jana
na Diwani wa Kata Miswaki Antony Makani kwa niaba ya wakazi wa Kata yake
alipokuwa akiwasilisha ombi kwa Wakala wa Maji safi na usafi wa mazingira
Vijijini (RUWASA).
Alisema kutokana na
umbali waliopo kutoka mradi wa bomba la Ziwa Victoria kuja Tabora hawatarajii kunufaika
na maji hayo , njia pekee ya kuwasaidia ni kutumia mabonde yanayowazunguka
kujengea mabwawa.
Makani alisema Kata hiyo
ina wakazi zaidi ya 14,000 ambao wanalazimika kutumia maji ya madibwi ambayo
yamechnganyikana na takataka mbalimbali ambazo zinaweza kuwasababishia magonjwa
mbalimbali ya mlipuko.
Alisema eneo hilo liko
katika ukanda wa Bonde la ufa ambao ni vigumu kupata maji kwa wingi kwa njia ya
visima badala yake ni kwa njia ya kutega maji ya mvua.
Kwa upande wa Meneja wa
RUWASA wilaya ya Uyui Meneja wa Wakala wa Maji safi na usafi wa mazingira
Vijijini (RUWASA) Wilaya ya Uyui Godfrey Shibiti alisema kuwa ili Serikali
ijenge bwawa lazima iangalie uwekezaji wa eneo husika ili kujiridhisha juu ya
uwepo wa maji ya kutosha na kudumu kwa mradi.
No comments:
Post a Comment