HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

February 25, 2020

WANAWAKE ACT-WAZALENDO KUCHAGUANA MACHI

Mauwa Mohammed, Zanzibar
 
CHAMA Cha ACT-Wazalendo kinategemea kufanya uchaguzi Mkuu wa viongozi wake katika ngazi ya Taifa mnamo mwezi Machi mwaka huu huku kukiwa na idadi kubwa ya wanawake waliochukua fomu  za kuwambia nafasi  hizo.
 
Miongoni mwa waliochukua fomu hizo ni Janet Fusi mwanamke ambae ameonekana kuwa shupavu mpenda mageuzi aliyechukua  fomu ya kugombea nafasi ya makamo mwenyekiti wa chama Taifa.
 
Akizungumza mara bada ya kuchukua fomu hiyo huko katika ofisi ya chama hicho iliyopo mtaa wa Vuga Mjini Zanzibar,  Janet alisema yeye ni mwanamke anaejiamini na kuwa anauwezo wa kuingia katika kinyanganyiro cha kugombea na nafasi hiyo.
 
“Nimechukua nafasi hii kwa sababu kikatiba inaniruhusu na nnao uwezo wa kuitendea haki nafasi hii”.
 
Janet aliwataka kina mama wenzake kujitokeza kwa wingi katika mchakato wa kugombea nafasi za uongozi kwani wanawake wameonekana kuwa na uwezo mkubwa wa kiuongozi.
 
Nae naibu katibu wa ngome ya wanawake wa chama hicho Zahra Ali Hamadi amesema amechukua nafasi ya ukatibu mkuu wa ngome ya wanawake kutokana na kuwa  anao uwezo wa kuongoza kwani ni mzowefu katika uongozi.
 
“Uzowefu wangu wa uongozi nilionao unanipa uwezo wa kuchukua nafasi ya juu zaidi kuliko niliyonayo hivi sasa”alisema nd, Zahra.
 
Hata hivyo alisema kwa kuwa chama chao cha ACT kimekuwa kwa kasi kubwa  na kimekuwa ni tishio kwa vyama vingine kinahitaji kupata viongozi imara na wadilifu ili waweze kufikia malengo yaliyokusudiwa katika kufikia demokrasia ya kweli.
 
Sambamba na hilo nd, Zahra alisema lengo hasa la kuchukua nafasi hiyo ya ukatibu mkuu ni kuwaunganisha wanawake na kuwashirikisha katika nyanja mbali za kimaendeleo yao ya kiuchumi.

Miongoni mwa wanawake waliochukua nafasi za uongozi ni kaimu katibu mkuu wa chama hicho Dorothy Semu ambae amechukua  fomu ya kugombea nafasi  ya ukatibu mkuu wa chama.
 
Kwa hapa kisiwa cha Unguja Wengine waliojitokeza katika kuchukua fomu zakugombea nafasi za uongozi ni Mashavu Bakari na Nawiye Abdalla waliochukua fomu ya kugombea nafasi ya Makamo mwenyekiti wa ngome ya wanawake na  Raisa Abdalla Mussa ambae amechukua fomu ya kugombea nafasi ya  naibu katibu mkuu ngome ya wanawake.
 
Wengine ni Fatma Abdulhabib Fereji Pavu Abdalla na Arafa Musa Uledi wamechukua fomu ya kugombea nafasi ya halmashuri kuu ya chama.

Chama cha ACT wazalendo  tokea kuanza chaguzi zake  wanawake wameonekana kujitokeza kuchukua nafasi za juu ikwemo wenyeviti makatibu na wajumbe katika ngazi za Matawi Wadi Majimbo , Mikoa na Taifa.

No comments:

Post a Comment

Pages