Mjane Zainabu Mkwama na mtoto wa marehemu Mume wake Julius Olomi wakiwa mahakamani wakipinga kutaka kuondolewa katika usimamizi wa mirathi.
Na Mwandishi Wetu
KESI ya kugombea mali za marehemu bilionea Jubilate Olomi imerejeshwa tena mahakamani kuu Kanda ya Moshi,baada ya mdogo bilionea huyo, Werandumi Ulomi kuomba Mjane wa bilionea huyo,Zainabu Mkwama kuondolewa kusimamia mirathi.
Werandumi kupitia Wakili wake,Joseph Ngiloi amewasilisha maombi ya dharura mahakama kuu kanda ya Moshi,kuomba mjane huyo, kuondolewa katika usimamizi wa mirathi wakimtuhumu kufuja mali za marehemu mume wake.
Maombi hayo, yametajwa leo jumanne Machi 3mbele ya jaji Thadeo Mwenempazi mahakama kuu kanda ya Moshi ambapo mawakili wa Mjane watajibu hoja za wafungua maombi kabla ya kupangwa kuanza kusikilizwa shauri hilo.
Akizungumza na blog hii jana, Wakili Ngiloi alisema wamelazimika kurejea mahakamani, baada ya kubaini mjane wa Bilionea huyo, kufuja mali za ndugu yao,ikiwepo kushindwa kuhifadhi kwenye akaunti maalum fedha za watoto wa marehemu.
"tulikubali kuingia katika mjadala ya kugawanya mali baada ya kuagizwa na mahakama kuu, lakini tumeshindwa kufikia muafaka"alisema
Hata hivyo, Mjane Zainabu akizungumza na mwananchi alipinga tuhuma hizo na kueleza chanzo cha mgogoro ndogo wa mumewe Werandumi na wakili Ngiloi , kukataa kusalimisha hati na mali mbalimbali na marehemu mumewe ili kutambuliwa.
"baada ya kuona wamegoma kusalimisha mali za marehemu, ikiwepo hati za viwanja na mashamba ili kuzikusanya, mimi na mtoto mkubwa wa marehemu tuliomba kuongezewa muda wa kukusanya mali na kesi hiyo itatajwa Machi 12 mwaka huu"alisema
Mei 28 mwaka jana,Mahakama kuu Kanda ya Moshi, imetupilia mbali maombi ya Werandumi Olomi, kutaka kusimamia na kukusanya mali ya marehemu kaka yake, pekeyake na kuwapa haki hiyo watu watatu, Mjane Zainabu Rashid na mtoto wa marehemu julius Olomi na Werandumi.
No comments:
Post a Comment