HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

March 07, 2020

Mwanamke ni kiungo katika uhifadhi wa mazingira

Catherine Kahuka (kushoto) na Gloria Wangeleja (kulia), wawakilishi kutoka taasisi ya PLPDF kupitia Shirika la Uhifadhi Mazingira Daniani (WWF), ofisi ya Tanzania wakipanda mtiti.

Na Asha Mwakyonde

SHIRIKA la Uhifadhi wa Mazingira  Duniani (WWF), ofisi ya Dar es Salaam Tanzania kwa kushirikiana na Taasisi ya Vodacom Tanzania imepanda miti mia moja na kuwatembelea akina mama waliojifungua katika Hospitali ya Taifa Muhimbili - Mloganzila  ikiwa ni kuelekea maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani ambayo hufanyika Machi 8, kila mwaka.

Upandaji miti huo ulienda sambamba na uchangiaji damu na utoaji zawadi kwa watoto waliozaliwa hospitalini hapo  ikiwa ni kujumuika pamoja na akina mama hao katika siku hiyo ya wanawake duniani.

Akizungumza jijini Dar es Salaam Machi 6, mwaka huu hospitalini hapo mara baada ya kufanya shughuli hizo Meneja Mawasiliano wa WWF, Joan Tanisa amesema kuwa shirika la uhifadhi mazingira kupanda  miti ni moja kati ya kazi zao za msingi.

Joan amesema mazingira yakiwa mazuri mama mwenye mzigo wa mkubwa wa kuilea familia yake  anaweza kupata nafuu na kwamba miti inapopandwa na kustawi vizuri  kutakuwa na upatikanaji wa maji ya kutosha  na mama huyo hatapata shida ya kutembea umbali mrefu kutafuta maji.

Amesema kuwa mwanamke ni kiungo katika suala la uhifadhi wa mazingira kwani shughuli nyingi anazozifanya zinahusiana na mazingira na kwamba ana nafasi ya kubwa ya kuelimisha familia yake juu ya uhifadhi huo.

 "Kwa wanawake wenzetu wa vijijini wabaolima, wanaokwenda kutafuta kuni na ndio wanaohudumia familia hivyo ndio mwalimu wa kwanza wa kuweza kutoa elimu ya uhifadhi mazingira,"amesema Joan.

Ameongeza  kuwa wamepanda miti maeneo mbalimbali  hapa nchini hivyo wameona wafanye kitu gani ambacho kitangusa  mwanamke moja kwa moja katika yale ambayo anayafanya  kila siku.

Naye Meneja Ruzuku na Mawasiliano wa Taasisi ya Vodacom Sandra Oswadi amesema taasisi hiyo ni ya kujitolea kwa jamii  na kwamba wamejumuika na akina mama hao waliojifungua  kwa kupanda miti na kutoa zawadi kwa watoto.

"Siku hii tumekuja kupanda miti ambayo imetokana na mkakati wetu wa miaka mitatu wa kutunza mazingira. Kwa mwaka wa kwanza tumedhamiria kupanda miti 70,000 ambao unaishia mwishoni mwa mwezi huu,"amessema

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Uunguzi na Ukunga kutoka hospitali ya Nuhimbili - Mloganzila Redemptha Matindi  ametoa shukrani kwa WWF na taasisi ya Vodacom  kwa kupanda miti na kuungana na wanawake waliojifungua na kulazwa hospitalini hapo

No comments:

Post a Comment

Pages