HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

March 07, 2020

Zaidi ya 250 wajitokeza kufanyiwa uchunguzi Siku ya Presha ya Macho Mloganzila

Daktari Bingwa wa Macho wa MNH-Mloganzila, Dk. Catherine Makunja, akimfanyia uchunguzi wa macho wa awali, Ashura Abdallah, aliyefika hospitalini hapo. (Na Mpiga Picha Wetu).

Mamia wamejitokeza kufanyiwa uchunguzi wa awali wa macho katika Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila katika maadhimisho ya Siku ya Presha ya Macho Duniani yenye kauli mbiu isemayo “Tokomeza Shinikizo la Macho lililojificha” lengo ikiwa ni kufanya uchunguzi wa macho, kupima presha ya macho, kutoa ushauri juu ya magonjwa ya macho pamoja na matibabu yake.

Ambapo imetajwa kuwa umri wa miaka 40 na kuendelea hukutwa na ugonjwa wa presha ya macho sababu ikiwa ni magonjwa ya kurithi katika familia, kisukari, unywaji pombe kupita kiasi, uvutaji sigara na matumizi ya dawa bila kufuata
ushauri wa daktari.
 
Hayo yamesemwa na Daktari wa Macho wa Hospitali ya Taifa Muhimbili- Mloganzila, Dkt. Catherine Makunja wakati akifafanua juu ya ugonjwa wa presha ya macho na kusema kuwa ugonjwa huu mara nyingi hauna dalili hivyo ni vema
watu wakajijengea tabia ya kufanya uchunguzi wa macho mara kwa mara.
 
“Tatizo la presha ya macho huwa mara nyingi linapoanza halina dalili na wagonjwa mara tu wanapofanyiwa vipimo huwa wanakutwa na ugonjwa huu ndio maana tunatoa hamasa kwa watu kuja kufanya uchunguzi mara kwa mara”
amesema Dkt. Makunja.
 
Sambamba na hilo Daktari wa Macho wa MNH-Mloganzila, Dkt. Judith Mwende amefafanua kuwa mbali na wagonjwa kufanyiwa uchunguzi wa macho na kugunduliwa kuwa na presha ya macho madaktari hufanya uchunguzi wa kina ili
kutambua aina ya presha ya macho aliyonayo mgonjwa.

Kwa upande wake mmoja wa watu waliojitokeza kufanyiwa uchunguzi hospitalini hapa leo, Bi. Nora Charles amewashauri watanzania kujitokeza kwa wingi kufanyiwa uchunguzi wa magonjwa mbalimbali na kupatiwa matibabu mapema.

No comments:

Post a Comment

Pages