HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

March 19, 2020

Rose: Idadi ya Wakunga iongezwe

Mratibu a Shirika lisilo la kiserikali la Utepe Mweupe (White Ribbon), nchini  Rose Mlay akizungumza jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa kampeni ya " Wanawake wanataja nini, Sikiliza na Chukua Hatua".


Na Asha Mwakyonde

MRATIBU  wa Shirika lisilo la kiserikali la Utepe Mweupe (White Ribbon), nchini  Rose Mlay ameiomba serikali kuongeza idadi ya wakunga katika vituo vya afya, zahanati na hospitali za mikoa ili akina mama wapate huduma nzuri pindi wanapojifungua.

Akizungumza jijini Dar es Salaam juzi wakati  wa uzinduzi wa Kampeni ya "Wanawake wanataka nini ,Sikiliza Chukua Hatua" iliyoandaliwa na Shirika hilo amesema katika uzazi kuna chabgamoto nyingi wakati wa kujifingua.

Mratibu huyo amesema wanatamani  kuona hospitali za Wilaya ziwe na wakunga 20, hospitali ya Rufaa na Mkoa wawe 102 wanaofanya kazi za ukunga tu lengo ni kuwaangalia akina mama wanaenda kujifingua kwa ukaribu zaidi.

"Tunaomba wizara ya afya iongeze wakunga wa katika kila kituo cha afya angalau wawe wakunga watano wanaofanya kazi ya ukunga tu kwani kwa sasa ukienda utakuta mkunga mmoja au wawili ambapo idadi ndogo ikilinganishwa na akina mama wanaojifungua kwa siku," ameeleza Rose.

Rose aneongeza kuwa utafiti walioufanya katika Mikoa 10 kwa kuwauliza wanawake 110,000 alisilimia 8.61 ya wanawake hao walitaka huduma za uzazi zenye heshima na utu.

Amesema  asilimia 8.99 walitaka madawa na vifaa ,asilimia 7.56 walitaka huduma zilizoboreshwa na ustawi na afya ya uzazi kwa ujumla,asilimia 7.32 na pia walitaka kuongezwa vituo vya afya vyenye ukamilifu na kwamba wengine  waliotaka ushauri nasaha, ufahamu kuhusua afya ya uzazi walikuwa 7.17.

Akizindua kampeni hiyo Mkurugenzi wa Huduma za Kinga wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Dk Leonard Subi kwa niaba ya Waziri mwenye dhamana Ummy Mwalimu amewaasa akina mama kujiepusha na vitengo vya kutoa rushwa Pindi wanapojifungua.

Mkurugenzi huyo amesema kila mtu ana  haki ya kupata huduma hivyo  kuendelea kutoa rushwa ni kurudisha maendeleo ya nchi nyuma.

Dk. Subi amesema  kuwa serikali inaendelea kuboresha huduma za afya ili kila mtu apate huduma huduma bora hivyo mwananchi kupata huduma ni haki yake.

Amesema  upatikanaji wa dawa umeongezeka ambapo kwasasa dawa muhimu zinapatikana kwa asilimia 94 huku chanjo zinapatikana kwa asilimia 98.

Hata hivyo amesema kuwa utafiti mdogo uliofanywa unaonesha vifo vitokanavyo na uzazi vimepungua kutoka 1744 mwaka 2018 hadi kufikia 1657 lwa mwaka 2019

Dk. Subi ameongeza kuwa katika  kipindi cha miaka minne serikali imeweza kujenga Hospitali 70 ambapo miaka zaidi ya 50 ya uhuru kulikuwa na hospitali 77 tu katika kila Mkoa mpya na kwamba serikali imejenga hospitali na vituo vya afya 540 vimejengwa na vingine kukarabatiwa.

"Tumeboresha Miundombinu ya vituo vya afya 361 lengo letu ni kuwasikiliza wanawake wanakochotaka hivyo idadi ya akinamama wanaojifungulia vituo vya afya imeongezeka mwanzo ilikuwa asilimia 63 lakini sasa wamefikia asilimia 79,"amesema Dk Subi.

Amesema ongezeko  hilo la dawa limetokea baada ya bajeti ya dawa kuongezwa kutoka Sh bilioni 30 hadi Sh bilioni 270.

Anesema kwa kushirikiana na Taasisi ya Taifa ya Magonjwa ya Binadamu (NIMR), Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS)na taasisi zingine za serikali na zisizo za kiserikali wanatarajia kukamilisha utafiti wa vifo vitokanavyo na uzazi.

Dk Subi pia amewataka wanaume kuwasikiliza wake zao nini wanachotaka hasa kipindi cha ujauzito ili kuwapunguzia mawazo.

No comments:

Post a Comment

Pages