HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

March 19, 2020

Corona yakwamisha ligi ya Ng'ombe

Katibu Mwenezi wa Kata ya Kivule Bihimba Mpaya (Chadema).
 

Na Asha Mwakyonde

KATIBU Mwenezi wa Kata ya Kivule kupitia  Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Bihimba Mpaya amesema ugonjwa wa Corona unaosababishwa na kirusi aina ya COVID-19 ambao tayari umeingia  nchini umezuia uazaji wa ligi ya ngo'mbe iliyopangwa kufanyika mwezi huu katika Kata hiyo

Akizungumza na Habari Mseto Blog, Machi 19 mwaka huu jijini Dar es Salaam Mpaya amesema kutokana na tamko lililotolewa hivi karibuni  na Waziri  Mkuu Kassim Majaaliwa la kutokuwepo kwa mikusanyiko ya watu kwa kipindi cha mwezi mmoja  ligi hiyo itapangwa tena baada ya kumalizika kwa  tamko hilo.

Katibu huyo alisema kuwa lengo la ligi hiyo ni kuwakusanya vijana pamoja ili waweze kuhahamiana na kuweza kushirikiana katika mambo mbalimbali ya kijamii pindi wanapofahamiana.

Mpaya aliongeza kuwa mbali na kufahamiana vijana hao kwa wenye vitendo vibaya kama uborsji, uvutaji bangi wataweza kubadilika kupitia vijana wenzao .

"Kwanza michezo ni afya pia vijana watakaoshiriki ligi hii ya  ng'ombe wakishinda watakunywa supu  lakini pia itawahamasisha wenye matendo maovu kuacha kabisa,"amesema Mpaya.

Mpaya alisema Kata hiyo ina mitaa minne ambayo ni Bombambili, Magole,Kerezange na Kivule.

Aliwataka vijana wa mitaa hiyo minne kuwa tayari kujitojeza kwa wingi kuwania ng'ombe huyo  ili wajiongezee kipato kwa timu itakayonda au kunywa supu kutokana na makubaliano yao.

No comments:

Post a Comment

Pages