Mkuu
wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri akifungua
kikao cha Bodi ya Barabara cha Mkoa wa Tabora.
Meneja
wa Wakala wa Barabara Tanzania(TANROAD) Mkoa wa Tabora Ndamiani Ndabalinze
akitoa mada jana wakati wa ufunguzi wa kikao cha Bodi ya Barabara cha Mkoa
wa Tabora.
Baadhi
ya wajumbe wa kikao cha kwanza cha Bodi ya Barabara cha Mkoa wa Tabora
wakifuatilia hotuba ya ufunguzi wa Kikao hicho.
Na Tiganya Vincent, Tabora
WAKALA wa Barabara Tanzania
(TANROD) Mkoa wa Tabora imewasilisha mapendekezo ya shilingi bilini 23.3 kwa
ajili ya matengenezo ya barabara.
Kauli hiyo imewasilishwa
jana na Meneja wa Wakala wa Barbara Tanzania (TANROADS) Mkoa wa Tabora Ndamiani
Ndabalinze wakati akitoa mada jana wakati wa kikao cha Bodi ya Barabara cha
Mkoa wa Tabora.
Alisema
fedha hizo zinajumuisha shilingi bilioni 21.1 toka Mfuko wa Barabara na
shilingi bilioni 2.2 kutoka Mfuko wa Maendeleo.
Ndabalinze alisema kuwa kwa barabara kuu wanatarajia
kutengeneza kilometa 759.9, matengenezo ya barabara za Mkoa kilometa 1,318.1 na
barabara za Wilaya zenye urefu wa kilometa 2,170.3.
Alisema kupitia miradi ya maendeleo wanatarajia
kukarabati kilometa 130.
Katika hatua nyingine Meneja wa TANROADS Mkoa wa
Tabora Ndabalinze alisema katika kipindi cha kuanzia Septemba 2019 hadi Februari,
2020, Ofisi hiyo imepeleka maombi ya shilingi bilioni 2.4 kwa ajili ya
kukarabati barabara zilizoathiriwa na
mvua.
No comments:
Post a Comment