HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

March 11, 2020

UKATILI WA KIJISIA WAONGEZEKA KAGERA

Jaji  Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Bukoba, Lucia Kairo (aliyevaa skafu), akizungumza na wananchi katika kilele cha Wiki ya Sheria  na Siku ya Wanawake duniani.

 
Na Alodia Dominick, Kagera

 Taasisi mbalimbali za serikali na zisizo za serikali zimeendelea kutoa elimu ya msaada wa kisheria kutokana na ukatili wa kijinsia kuendelea kupanda katika mkoa Kagera kwa 40 asilimia.

Takwimu zinaonyesha kuwa, kwa mwaka 2018/2019 watu waliofanyiwa ukatili kwa mkoa wa Kagera ilikuwa ni asilimia 40, chini ya miaka 15 hadi 49 walifanyiwa ukatili wa kimwili sawa na asilimia 17, miaka 15 hadi  49 walifanyiwa ukatili wa kingono sawa na asilimia 30 hawa ni walioolewa na asilimia 54 walipata msaada wa kipolisi au wa kisheria.

Ukatiri huo ni pamoja na mimba za utotoni, ukatiri kwenye ndoa, unyanganyi wa ardhi na ubakaji, na kutokana na msaada wa kisheria unaotolewa na mashirika mbalimbali mkoani humo jamii imeendelea kuelimishwa sehemu ya kutoa taarifa wanapokumbwa na ukatiri.

Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Bukoba, Lucia Kairo, katika kuhitimisha wiki ya sheria iliyoanza machi 3 mwaka huu  na kuhitimishwa machi 8 mwaka huu ambayo pia ilikuwa siku ya mwanamke duniani iliyofanyika kimkoa katika wilaya ya Bihalamro alisema msaada wa kisheria uendelee kutolewa kupitia taasisi za serikali na zisizo za serikali ili kuwapa wananchi uelewa wa kisheria ili pale wanaponyanyaswa wajue ni wapi waweze kupata haki yao.

Akitoa takwimu za waliopewa msaada wa kisheria katika wiki hiyo mwakilishi wa mawakili wa kujitegemea Jovin Rutainulwa alisema katika wiki ya sheria iliyozinduliwa wilayani Karagwe idadi kubwa ya watu migogoro yao ilikuwa inahusiana na ardhi ambapo watu 334 wilayani Karagwe waliopata msaada ya kisheria kati yao 56 walikuwa na migogoro ya ardhi, wilaya ya Ngara waliopata msaada wa kisheria walikuwa 140 kati ya hao 38 ilikuwa migogoro ya ardhi na wilaya ya Bihalamro waliopata msaada wa kisheria walikuwa 238.

Mkurugenzi wa Mtandao unaotoa elimu ya kisheria Tanzania TANLAP, Christina Ruhinda, alieleza kwamba, mtandao wao una mashirika 78 hapa nchini ambao hutoa msaada wa kisheria na kila wilaya katika mkoa wa Kagera wameanzisha klabu za wanafunzi zinazopinga unyanyasaji ambazo hutumika katika kutoa elimu kwenye mikusanyiko ya watu.

Naye Katibu Tawala Mkoa wa Kagera, Faustine Kamzora, aliyaomba mashirika mbalimbali kuendesha kampeni ya hedhi salama ili kuendelea kumlida mtoto wa kike.

Aidha meneja wa world vision Bukoba,  Juliana Charles, alieleza kwamba shirika hilo linatoa huduma mbalimbali kwa wanawake na watoto wa kike ikiwa ni pamoja na elimu, kwa kutoa mafunzo mbalimbali yanayohusu kilimo na lishe bora, wanatoa taulo za kike kwa wanafunzi na elimu kuhusu hedhi salama. 

No comments:

Post a Comment

Pages