HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

March 11, 2020

MKOA WA KAGERA WAPOKEA VITABU VYA KIADA KUTOKA SERIKALINI

Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Brigedia Jenerali Marco Gaguti, akikabidhi vitabu kwa Ofisa Elimu Mkoa wa Kagera, Juma Mhina.


Na Alodia Dominick, Bukoba


 Zaidi ya vitabu  175,000 vya kiada vimetolewa na serikali hapa nchini kupitia Tawala za mikoa na serikali za mitaa (TAMISEMI) kwa shule za msingi na sekondari mkoani  Kagera.

Vitabu hivyo vimepokelewa leo na Mkuu wa Mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali Marco Gaguti, baada ya kusafirishwa hadi mkoani hapa na mkuu huyo kuvikabidhi kwa ofisa elimu wa mkoa huo Juma Mhina.

Akikabidhi vitabu hivyo mkuu wa mkoa Brigedia Gaguti amesema kuwa kutokana na kutolewa vitabu hivyo ni imani yake kuwa elimu mkoani Kagera kwa shule za msingi na sekondari itaboreshwa na baada ya vitabu kupokelewa visambazwe ndani ya siku tatu katika shule zote za mkoa huo.

“ Vitabu hivyo vitumike kwa malengo yaliyokusudiwa kubwa Zaidi kwa walimu na wanafunzi wakatumie vitabu hivi kwa matumizi endelevu vikatoe msaada wa kujifunza kwa urahisi zaidi  mvitunze na mvitumie kwa muda mrefu maana serikali imetumia muda mrefu kuvichapisha’’ Alisema Generali Gaguti.

Vilevile ameishukuru serikali kwa kutoa vitabu hivyo na kusema kuwa ufauru katika mitihani ya mwisho kwa upande wa shule za sekondari na msingi utaweza kuongezeka.

Ofisa elimu mkoa wa Kagera Juma Mhina amesema, vitabu vilivyotolewa ni 175,253 vya kiada kwa shule za msingi na sekondarikwa darasa la sita, Kidato cha kwanza,kidato cha pili, kidato cha nne na cha sita na  vitabu vya wanafunzi wenye mahitaji maalum.

Mhina ameeleza kuwa tangu januari mwaka huu darasa la sita hawakuwa na vitabu vya kiada vya kutumia  hivyo kutokana na vitabu hivyo kuletwa wataanza kutumia vitabu hivyo na kuwa vitagawiwa kwa halmashauri zote nane za mkoa wa Kagera.

Naye Avion Emmanuel mwanafunzi kutoka shule ya sekondari ya Wasichana Rugambwa amesema kutokana na vitabu vilivyoletwa vya wanafunzi wenye uhitaji maalumu vitaweza kuwasaidia kujisomea wenyewe hata kama hawana mwalimu wa kuwafundisha.

No comments:

Post a Comment

Pages