HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

April 24, 2020

General Petroleum yatoa vyakula kwa kaya maskini 1,500 Dar es Salam, Bagamoyo

Na Suleiman Msuya

KAMPUNI ya General Petroleum ya jijini Dar es Salaam imetoa vyakula vya aina mbalimbali vyenye thamani ya Sh.Milioni 50 kwa kaya zaidi 1,500 za kipato cha chini ili ziweze kukabiliana na ugumu wa maisha katika kipindi hiki cha mapambano dhidi ya ugonjwa wa COVID-19 na Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

Msaada huo umetolewa na Meneja Mauzo wa Kampuni hiyo Zafar Khan wakati akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam.

Alisema GP ni kampuni ambayo inapenda kusaidia jamii hivyo imeamua kuungana na Serikali katika kipindi hiki cha janga la virusi vya corona kwa kuwapatia wananchi wanyonge chakula na mafuta.

Khan alisema kwa sasa wemetoa msaada kwa kaya 1,500 za jijini Dar es. Salaam na Bagamoyo hivyo wanaamini wataweza kusaidi kiasi kuondoa ugumu wa maisha kwa familia.

"Sisi kama wadau wa maendeleo ndani ya wilaya ya Temeke na Tanzania na Tanzania kwa ujumla tumeamua kutoa msaada huu wa vyakula na mafuta kwa kaya 1,500 kipindi hiki cha mapambano ya ugonjwa wa COVID-19 lakini pia vitawasaidia kwa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani," alisema.

Akizungumza baada ya kupokea msaada huo Katibu Tarafa ya Mbagala wilayani Temeke  Betha  Minga wakati akipokea vitu hivyo  alisema wanawashukuru Kamapuni ya GP kwa kuwakumba wanyonge katika kipindi hiki.

Minga alisema GP ni wadau wakubwa wa maendeleo wilayani hapo na kuwataka waendelee na moyo huo huo.

Aliema awali kabla ya kutoa msaada huo ambao unajumla ya ya thamani ya shilingi zaidi ya Milioni 50 za kitanzania walishatoa vitakasa mikono, na Barakoa kwa ajili wananchi wa kata 23 za Manispaa hiyo ya Temeke.

"Binafsi kwa niaba ya mkuu wa Wilaya ya Temeke tunawashukuru watu hawa kwani katika Wilaya yetu wamekuwa na msaada mkubwa Sana Mara zote wamekuwa ni watu wakujitoa Sana hivyo tunawashukuru Sana na msaada huu unakwenda kwa watu waliokusudiwa ."alisema Minga.

Alisema vifaa hivyo vinakwenda katika kata zote zilizopo katika Wilaya ya Temeke na kila kata watapata vifurushi 20 na tayari tulishaainisha wanaostahiki kupata hususani katika kipindi hiki ambacho ndugu zetu waislamu wanaaza mfungo wa mwezi mtukufu wa ramadhani..

No comments:

Post a Comment

Pages