NA TIGANYA
VINCENT
Baraza la Taifa la watu wanaoishi na VVU (NACOPHA)
limetoa vifaa vyenye thamani ya shilingi
milioni 26 kwa Mkoa wa Tabora kwa ajili ya watu wanaosihi na virusi
vinavyosabisha Ukimwi kujikinga na kudhibiti kuenea kwa Virusi vya Corona.
Hatua hiyo inalenga kuwawezesha jamii ya watu wanaoishi na VVU na
jamii inayokuwa karibu nao kuweza kuvitumia katika kuchukua hatua za kujikinga
na kupata maambukizi ya ugonjwa wa Covid -19.
Vifaa hivyo vimekabidhiwa jana mjini Tabora na Mtendaji
Mkuu wa NACOPHA Deogratis Rutatwa na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri kwa
niaba ya Halmashauri zote.
Alisema wametoa sabuni za kunawiana mikoni, vitakasa
mikono, vidonge vya kuweka katika maji ya kunawiana . Detto na barakoa.
Rutatwa alisema wameamua kutoa msaada huo ambao
wamesaidia na Shirika la Misaada la Watu wa Marekani(USAID) chini ya kauli mbinu hebu tuyajenge tufiku
95-95-95 ili kuungana na jitihada za Serikali za kukabiliana na janga la Corona
kwa watu wanaoishi na VVU.
Alisema pamoja na Mkoa wa Tabora pia wametoa vifaa vya
aina hiyo Kigoma, Shinyanga, Geita, Kagera, Mwanza na Mara ili viweza kuwasaidia
watu wanaoishi na VVU kujingana
na Corona.
Akipokea vifaa hivyo kwa niaba ya Halmashauri nane za
Mkoa wa Tabora, Mkuu wa Mkoa huo Mwanri aliishukuru NACOPHA kwa kujali na kuona
umuhimu wa kusaidia kundi hilo katika kukabiliana na janga la Corona.
Alitoa wito kwa Mashirika mengine kusaidia vifaa kwa
watu wenye mahitaji maalumu kama vile walemavu ili waweze kujinga na Corona.
Mwanri alisema jamii ya watu wenye ulemavu wakati
mwingine inahitaji msaada wa mtu wa pili katika kufanya shughuli mbalimbali na
hivyo wasipokuwa na vifaa kama vile barakoo, vitakasa mikono wanaweza kupata
maambukizi ya Corona.
Aliwaonya watu watakaopewa vifaa hivyo kuvitumia kwa
makusudi yaliyokusudiwa na sio kutumia nje ya malengo.
No comments:
Post a Comment