Na Tiganya Vincent
MKUU wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri ameagiza viongozi
wa Halmashauri mbalimbali kuanza kuchukua hatua dhidi ya watoto wote
wanaodhurura ovyo mitaani na kuhatarisha maisha yao baada ya shule kuwa
zimefungua kwa ajili ya kuwakinga na Corona.
Alisema haiwezekani Serikali ilifunga Shule kwa ajili
ya kuwaondoa watoto katika msongamano bado kuwa baadhi yao wanaonekana katika
mitaa wakiuza karanga, mchicha na wengine wakiwasaidia wazazi wao kuuza chakula
katika migahawa ya chakula.
Mwanri alitoa kauli hiyo jana wakati kipindi maalumu
cha kuwaelimisha wawakilishi wa watu wenye ulemavu jinsi ya kukabiliana na
janga la Corona ambalo kilikuwa pia kikitangwa na redio za Kijamii mkoani hapa.
Alisema watoto wanatakiwa kukaa majumbani huku
wakifuatilia masomo kwa njia ya vyombo vya habari na wengine wakipitia vitabu
mbalimbali ili kujikumbusha walichofundishwa.
Aidha Mkuu huyo wa Mkoa alisema pindi janga la Corona
litakapokuwa limemalizika na Shule kufunguliwa wanafunzi wote wa kike ni lazima
wapimwe ujauzito baada ya kuwekuwepo na tuhuma kuwa baadhi yao wameonekana
katika maeneo ya nyumba za kulala wageni.
Alisema watakaobainika kuwa na ujauzito watachukuliwa
hatua kali ikiwemo wazazi wao na mtu atakayekuwa akituhumia kumrubuni na kumpa
ujauzito.
Mwanri aliwataka wazazi kuhakikisha wanakuwa karibu na
watoto wao katika kipindi hiki ambacho hawako shuleni ili kuwalea katika
maadili mema.
Awali Mratibu wa Wajasiriamali Mkoa wa Tabora Ashura
Mwanzembe alisema baadhi ya watoto wa kike wamekuwa wakitumika kuuza karanga,
mahindi ya kupika kuingia katika nyumba za kulala wageni kwa madai ya kutafuta
wateja wa bidhaa wanauza huku wakijiweka katika hatari.
Alisema hivi karibuni alilazimika kumchapa binti mmoja
aliyekuwa akiuza karanga baada ya kumuona akitoka katika nyumba ya kulala
wageni kwa kisingizio kuwa alikuwa akitembeza karanga ndani.
Ashura aliwaomba wazazi kuacha kuwafanyisha kazi za
kuuza mchicha , karanga na vitu vingine kwa kuwa watu wenye nia mbaya wamekuwa
wakiwarubuni kwa kujifanya wananunua vitu vyote kwa mkupuo kwa niaba kuwataka
kimapenzi huku wanawaharibia maisha.
Baadhi
ya watu wenye ulemavu wakipa elimu ya kujikinga na Corona kutoka kwa
wataalamu na viongozi mbalimbali wa Mkoa wa Tabora.
Mkuu
wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri akitoa ufafanuzi jana kwa watu wenye
ulemavu wakati wa muendeleza wa utoaji wa elimu ya kujinga na Corona kwa
makundi mbalimbali Mkoani humo. Elimu hiyo ilikuwa ikirushwa na Redio
mbalimbali za Mkoa huo. (Picha na Tiganya Vincent).
No comments:
Post a Comment