Madereva hao ni: Abdalla Said, Mohamed Salehe, Twaliha
Mfinanga, Ramadhani Iddy na Adamu Gunza ambao wameibuka kidedea baada ya kufanya
miamala ya juu zaidi kupitia Mastercard QR tangu kuzinduliwa kwa kampeni hiyo.
NMB, kwa kushirikiana na Mastercard ilizindua huduma
ya Mastercard QR mwanzoni mwa mwaka jana ikiwa na lengo la kumwezesha abiria wa
bodaboda kulipa nauli kwa kutumia simu za mkononi na fedha hizo kwenda moja kwa
moja kwenye akaunti ya NMB ya dereva husika.
Akizungumza wakati wa
hafla ya makabidhiano ya zawadi iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana, Kaimu
Afisa Mkuu wa Fedha wa NMB, Benedicto Baragomwa ameisisitiza jamii kufahamu
umuhimu wa kutumia mfumo wa Mastercard QR hususani kipindi hiki ambacho dunia
inapitia kwenye mlipuko wa ugonjwa wa ‘COVID-19’ unaosababishwa na virusi vya
corona.
“Ukilipia nauli yako ya
bodaboda kwa mfumo huu abiria na dereva wanapunguza uwezekano
wa kupata au kusambaza ugonjwa wa COVID-19 kwa kuwa hakuna matumizi ya noti. Benki
ya NMB ina mifumo rafiki ya kidigitali ya kuwawezesha wateja wetu kupata huduma
zote za kukamilisha miamala kupitia simu zao za mkononi, ikiwa ni jitihada za
kusogeza huduma karibu zaidi kwa wateja,” amesema Baragomwa.
Kaimu Afisa Mkuu wa Fedha wa Benki ya NMB, Benedicto Baragomwa akimkabidhi kadi ya pikipiki, Abdallah Juma wakati wa hafla ya makabidhiano ya zawadi kwa washindi iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Naye Mkurugenzi wa Mastercard
Afrika Mashariki, Frank Molla ameongeza kuwa ushirikiano wao na Benki ya NMB
umelenga kuwasaidia wafanyabiashara kupokea malipo kwa mfumo wa kidijitali na
kuwezesha miamala kufanyika kwa njia salama, rahisi na kutohitaji kuwa na pesa
taslimu.
Hadi sasa kampeni hiyo
imewafikia waendesha bodaboda 4,855, ikiwa ni safari ya kuwafikia bodaboda 75,000
nchi nzima ifikapo mwishoni mwa mwaka. Hadi sasa zaidi ya bodaboda 100
wamejishindia zawadi mbali mbali zikiwemo elfu hamsini zinazotolewa kila wiki, simu
na watano ambao wamejishindia leo pikipiki.
No comments:
Post a Comment