HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

April 29, 2020

TMA: Mvua ipo hadi Mei Mosi


Na Irene Mark

MAMLAKA ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa tahadhari na angalizo la mvua kubwa kwa siku tatu kwenye baadhi ya maeneo ya nchi hasa ukanda wa Pwani ya Bahari ya Hindi na visiwa vya Unguja na Pemba.

Tahadhari na angalizo hilo lenye uwezekano mkubwa wa kutokea ilitolewa jana usiku na Ofisi ya Uhusiano ikibainisha kwamba mvua hiyo inatarajiwa kiendelea kunyesha hadi Mei Mosi mwaka huu.

Kwa mujibu wa mamlaka hiyo tahadhari imetakiwa kuchukuliwa kwa wakazi wa baadhi ya maeneo ya Jiji la Tanga na visiwa vya Unguja na Pemba.

"Hii ni taarifa ya hali mbaya ya hewa kuanzia Machi 27 hadi Mei Mosi hivyo ni muhimu kwa wananchi kuchukua tahadhari ya kuhakikisha wanasafisha maeneo yao ili kuruhusu maji ya mvua kutiririka yakituama yatasababisha mafuriko na mazalia ya mbu.

"Huu ni msimu wa masika kwa hiyo mvua ipo... nawashauri sana wananchi kuzingatia zaidi taarifa hizi za muda mfupi ili kujiepusha na athari za mvua," alibainisha Meneja wa Uhusiano wa TMA, Monica Mutoni alipozungumza na Habari Mseto Blog leo Machi 29.

Aliitaja mikoa iliyopewa angalizo la mvua kubwa kuwa ni Dar es Salaam, kaskazini mwa Mkoa wa Lindi na Pwani vikiwepo  visiwa vya Mafia.

No comments:

Post a Comment

Pages