HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

May 20, 2020

FMJ kuuza vifaa vya ujenzi kwa mnada

  Meneja Mauzo wa Kampuni ya Vifaa vya Ujenzi ya FMJ, Frederick Sanga, akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mnada wa vifaa vya ujenzi utakaofanyika Mei 30 mwaka huu katika ofisi za FMJ Buguruni Kisiwani Ilala jijini Dar es Salaam. (Picha na Suleiman Msuya).
Meneja Mauzo wa Kampuni ya Vifaa vya Ujenzi ya FMJ, Frederick Sanga,  akionesha baadhi ya vifaa vya ujenzi vitakavyouzwa kwa mnada Mei 30, 2020.


NA SULEIMAN MSUYA

KAMPUNI ya Uuzaji Vifaa vya Ujenzi FMJ Hardware Limitedi, ya Buguruni Kisiwani wilayani Ilala jijini Dar es Salaam inatarajia kufanya mnada wa vifaa vya ujenzi kwa njia ya mtandao siku ya Jumamosi Mei 30 mwaka
huu.

Hayo yamesemwa na Meneja Mauzo wa Kampuni hiyo, Fredrick Sanga, wakati akizungumza na waandishi wa habari jana ofisini kwake jijini Dar es Salaam.

Sanga alisema kampuni imeamua kuja na mbinu mpya ya kuuza bidhaa zake katika kipindi hiki cha maambukizi ya virusi vya corona vinavyosababisha ugonjwa wa COVID-19 ili kuendelea kushika soko la bidhaa za ujenzi nchini.

Alisema kupitia mnada mtandaoni wateja wao wataweza kupata bidhaa za ujenzi kwa bei rahisi hivyo kuwataka wateja na rejareja na jumla kujitokeza kwa wingi kununua bidhaa.
“Tumekuwa tukifanya biashara kila siku bila tatizo ila sasa tumeamua kuja na mbinu mpya yam nada ambapo tutaanza Jumamosi ya Mei 30 mwaka huu hapa ofisini kwetu Buguruni Kisiwani naamini wateja watanufaika,” alisema.

Meneja huyo alisema lengo la kutumia mbinu hiyo ni kuunga mkono jitihada za Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais John Magufuli katika kupambana na COVID-19 kwa wateja kupata bidhaa bila kufanya mikusanyiko.

Alisema bidhaa zitakazouzwa ni pamoja na bati, nondo, rangi, bomba na vifaa vyote ambavyo vinahusika na ujenzi kwa kuzingatia ubora uliothibitishwa na Shirika la Viwango Tanzania (TBS).

Sanga alisema kwa wateja ambao watataka kufuatilia mnada huo mubashara utarushwa kupitia Tanzanite TV Online, Ayo TV, Global TV, Dar Mpya TV Online na Icon TV.

“Tunawakaribisha wananchi kushiriki mnada huu wa aina yake kwani watapata bidhaa bora kwa ajili ya ujenzi kutoka kwa kampuni bora ya uuzaji vifaa hivyo,” alisema.

Meneja huyo alisema utaratibu huo mpya wa kufanya mnada katika kuuza bidhaa unatarajiwa kuendelea kwa siku zijazo lengo ni kukidhi hitaji la wateja wao.

No comments:

Post a Comment

Pages