Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uhusiano wa Halotel, Mhina Semwenda, akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa Duka la Kampuni hiyo Wilaya ya Kigamboni jijini Dar es Salaam.
Meneja wa Duka la Halotel Wilaya la Kigamboni, Harriet Maduhu, akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa Duka la Kampuni hiyo Wilaya ya Kigamboni jijini Dar es Salaam.Mkurugenzi wa Halotel Kanda ya Dar es Salaam na Pwani, Tran Nhat Dong, akitoa hotuba yake.
DAS wa Kigamboni, Rahel Mhando, akizungumza katika hafla hiyo.
Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Hashim Mgandilwa, akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Duka jipya la Halotel.
Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Hashim Mgandilwa, akipata maelezo ya duka hilo.
Keki.
Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Hashim Mgandilwa, akikata keki wakati wa hafla ya uzinduzi wa duka la Halotel Kigamboni.
DC Hashim Mgandilwa akiteta jambo na Tran Nhat Dong.
Shampeni ikifunguliwa.
DC Hashim Mgandilwa (kulia), akifurahia jambo na Mkurugenzi wa Halotel Kanda ya Dar es Salaam na Pwani, Tran Nhat Dong (katikati) na Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uhusiano, Mhina Semwenda.
NA HAPPINESS MNALE
KAMPUNI ya Mawasiliano ya Halotel imezindua tawi jipya la kutoa huduma katika Wilaya ya Kigamboni, jijini Dar es Salaam.
Akizungumza leo jijini Dar es Salaam, Meneja wa duka la Halotel Wilaya la kigamboni, Harriet Maduhu, alisema kwamba lengo la kufungua ofisi hiyo ni kusogeza huduma kwa wananchi.
Alisema kwamba duka hilo litatoa huduma zote za Halotel, ikiwemo kuuza simu, vocha na hata kuunganisha bando na kuuza modemu.
"Mwanzoni ilikuwa mpaka uvuke upande wa pili ama uende Temeke na Mbagala, lakini sasahivi huduma zote zitapatikana hapa hapa na wahudumu wapo wa kutosha, hivyo wakazi wa kigamboni ni wakati wao kuchangamkia fursa, tuna zawadi nyingi pia," alisema Harriet.
Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Hashim Mgandilwa, aliisifu Halotel kwa kuchangamkia fursa na kufungua tawi la Halotel Kigamboni.
Mgandilwa alisema kwamba kupitia tawi hilo vijana 20 watapata ajira ikiwemo promosheni mbalimbali za Halotel.
Aidha aliwataka wananchi kuiunga mkono Halotel kwani huduma zao ni nafuu na za haraka.
No comments:
Post a Comment