Na Suleiman Msuya
MBUNGE
wa Viti Maalum mkoa wa Iringa, Rita Kabati, ameiomba Serikali kuongeza
kodi ya ushuru wa bidhaa ya maziwa kutoka nje ili kulinda viwanda vya
ndani.
Aidha, Kabati
ameipongeza Kampuni ya Kuzalisha Maziwa ya ASAS ya mjini Iringa kwa
kutumia fursa ya kuongeza ushuru wa bidhaa kwa kuzalisha maziwa mengi.
Kabati
ametoa ombi na pongezi hizo Bungeni jiini Dodoma wakati akichangia
Bajeti ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi iliyowasilishwa na Waziri wa Luhaga
Mpina jana.
Mbunge huyo
wa Viti Maalum alisema Waziri Mpina na wasaidizi wake wameweza kumpaisha
Rais John Magufuli kupitia Wizara hiyo hivyo wanapaswa kuongeza nguvu.
"Tunaiomba
Serikali iongeze ushuru wa bidhaa kwa maziwa yanayotoka nje ili kulinda
viwanda vya ndani bei iwe chini viweze kujiendesha kwa faida," alisema.
"Wananchi
wengi wanaridhika na utendaji wa Wizara na Rais Magufuli hivyo nina
imani watamchagua tena kwa kura nyingi," aliongeza.
Mbunge
huyo alisema Wizara ya Mifugo na Uvuvi imejitahidi kukuza sekta hiyo
hivyo ombi lake ni ushuru wa bidhaa kuongezwa ili kukuza viwanda hasa
vya maziwa.
Alisema sekta hiyo ni muhimu katika kukuza uchumi wa nchi na wananchi kwa kuwa inashirikisha kundi kubwa la wavuvi na wafugaji.
Kabati
alisema iwapo ushuru wa bidhaa utaongezwa wawekezaji wa nje ambao
wamekuwa wakiingiza maziwa kutoka nje wataacha na kutumia yanazalishwa
hapa nchini.
"Wawekezaji
wanaingiza maziwa kutoka nje na kuuza bei mdogo na kuuwa viwanda vyetu
vya ndani. Hili halikubaliki lazima tuongeze ushuru wa bidhaa," alisema.
Mbunge
huyo alitolea mfano Kampuni ya ASAS ya mkoani Iringa ambayo imetumia
fursa ya kuongeza ushuru wa bidhaa na kuzalisha maziwa mengi
yanayotumika nchini.
"ASAS
imeweza kuinua kipato cha wafugaji wadogo wadogo wa Iringa, Njombe na
Mbeya. Lakini ameenda mbali kwa kuwakopesha ng'omba wa maziwa na
ukiangalia yote haya ni uamuzi wa Serikali kuongeza ushuru wa bidhaa,"
alisema.
Aidha, Kabati alisema Kampuni ya ASAS, imekuwa akitoa mchango mkubwa kwa kijamii ya mkoa huo.
"Mfano
amejenga jengo la damu salama, jengo la ustawi wa jamii ,amekuwa akitoa
maziwa kwa shule zote za Iringa sasa hivi ametoa vifaa na mashine na
vifaa ya kusaidia madktari na wauguzi, barakoa, ndoo na sanizer maeneo
ya masoko," alisema.
Kabati
alisema Serikali inapaswa kuunga mkono jitihada za wawekezaji wazawa
kama ASAS ili kuvutia wengine kuwekeza katika sekta ya viwanda vya
maziwa.
No comments:
Post a Comment