Kamanda wa Kikosi cha Zimamoto na Uokoaji Mkoa
wa Kagera, Hamis Dawa.
Na Lydia Lugakila, Kagera
Jeshi la Zimamoto
na Uokoaji mkoani Kagera limefanikiwa kuopoa mwili wa mtoto Mwenye umri wa
mwaka mmoja aliyefahamika kwa jina la Baraka Mwombeki mkazi wa eneo la Nyamkazi
manispaa ya Bukoba uliokutwa umetumbukia katika dimbwi la maji lililotokana
na mvua zinazoendelea kunyesha.
Kwa mujibu wa Kamanda wa Kikosi cha Zimamoto na Uokoaji Mkoa
wa Kagera, Hamis Dawa, taarifa za kuzama maji kwa mtoto huyo zimetolewa Mei 13
mwaka huu majira ya saa moja usiku
kutoka kwa askari wa zimamoto waliokuwa doria.
Askari hao wamedai
kuwa wameuona mwili wa mtoto huyo katika dimbwi la maji eneo la nyamkazi katika
manispaa ya bukoba, na kulazimika kwenda kuuopoa.
Dawa amesema
mazingira yanaonesha mtoto huyo alitumbukia katika dimbwi wakati akicheza, huku
mama mzazi wa mtoto huyo aliyetambulika kwa jina la Gisela mwombeki akishindwa kuelewa
mazingira aliyopo mtoto huyo.
No comments:
Post a Comment