Mkuu wa Mkoa wa Tabora
Aggrey Mwanri (katikati), akipokea msaada wa ndoo mbili zinazoruhusu mtu kunawa bila
kushika kutoka kwa Meneja wa Shirika la Kuhudumia
Viwanda Vidogo-SIDO-Mkoani Tabora, Samwel Neligwa (mwenye T-shirt ya rangi ya chungwa). (Picha na Tiganya Vincent).
Tiganya Vincent
MKUU wa Mkoa wa Tabora,
Aggrey Mwanri, ameagiza maeneo yote yanayotoa huduma kama vile sokoni na stendi
kufungwa vipaza sauti ili watu wanaofanyika kazi maeneo hayo waendelea kupata
elimu ya kujikinga na Covid -19.
Hatua hiyo inalenga
kuhakikisha wasafiri na wafanyabiashara wanaokuwepo katika maeneo hayo wanapata
elimu sahihi ya kukabiliana na kujikinga virusi vya Corona.
Mwanri alitoa kauli hiyo
jana wakati alipokutana na viongozi wa masoko , Stendi na wajane wakati
akiongoza timu ya wataalamu wa afya kutoa elimu ya kujikinga na covid -19.
Alisema kuwa kila siku
Redio zilizopo mkoani Tabora kupitia uongozi wa Mkoa na wataalamu wamekuwa
wakiendesha vipindi vya elimu ya kujikinga na virusi vya Corona kwa wakazi wa
Tabora.
Mwanri aliutaka uongozi
wa Manispaa ya Tabora na Halmashauri zote mkoani humo kuhakikisha wanafunga
vipaza sauti katika maeneo ya biashara na kuendelea na matangazo ya magari
mitaani ya kuwaelimisha wananchi kuchukua hatua za kujikinga na Virusi
vinavyosababisha Covid-19.
Aidha Mkuu huyo wa Mkoa
wa Tabora amewaagiza Watendaji wa Vijiji kuwatangazia wananchi katika maeneo
yao kufungulia Redio zilizopo Mkoani humo ili waweze kupata elimu sahihi ya
kukabiliana na virusi vya Covid -19.
Alisema Redio zilizopo mkoani Tabora kila siku zimekuwa zikitoa muda kwa watalaamu wa sekta ya afya
kuelezea mikakati na mbinu mbalimbali ambazo wananchi wanatakiwa kuchukua ili
kujilinda wasiweze kupata maambukizi ya Corona.
Katika hatua nyingine
Mkuu huyo wa Mkoa ameagiza Mamlaka ya Maji safi Tabora (TUWASA) kuhakikisha
maeneo ya shughuli nyingi kama vile sokoni na stendi kunakuwepo na maji ya
kutosha wakati ili watu waweze kunawa mikono.
No comments:
Post a Comment