Na Mwandishi Wetu
WAZIRI wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe (pichani) amezindua mfumo wa
majaribio wa ukatishaji tiketi wa mabasi kwanjia ya
mtandao huku akieleza kuwa njia hiyo italeta tija kwa
serikali,abiria,na wamiliki wa mabasi.
Akizungumza
jana mara baada ya uzinduzi huo Mhandisi Kamwelwe alisema mfumo wa
ukatishaji tiketi kwanjia ya mtandao utaondoa upotevu wa mapato kwa
wasafirishaji ambayo mara nyingi hupotelea katika mikono ya wapiga debe.
"Utawawezesha
wasafirishaji kukopesheka kwa urahisi kwani taarifa za miamala yao zitaakisi
moja kwa moja katika mabenki,pia utasaidia kuongezeka kwa uwekezaji katika
sekta kutokana na kuongezeka kwa mapato"alisema .
Mhandisi Kamwelwe
alisema kwa upande wa abiria matumizi ya mtandao katika ukatishaji tiketi utawaondolea
abiria mlolongo wa kufunga safari kwenda vituo vya mabasi siku moja kabla ya
safari waajili ya kukata tiketi.
"Pia utaondoa
kero za abiria kubughudhiwa kwenye vituo vya mabasi na kufanya usafiri huu kuwa
na heshima,utakomesha vitendo vya upandaji holela wa nauli hasa kipindi cha
mwisho wa mwaka "alisema.
Alisema kwa upande
wa serikali mfumo huo utawezesha kupatikani kwa taarifa muhimu zenye kusaidia
serikali kufikia maamuzi sahihi kwakuwa ndio kitovu cha usafirishaji nchini.
"Mfumo huu
utaisaidia Mamlaka ya Usafiri Ardhini (LATRA) kutambua idadi ya watu
wanaosafiri kwenda maeneo mbali mbali hivyo LATRA itapanga huduma za usafiri
kulingana na mahitaji ya eneo ya njia husika,mamlaka zinazohusika zitakuwa na
uwezo wa kupanga sera za usafirishaji na ujenzi wa miundombinu kutambua maeneo
ya kipaumbele ya usafirishaji"alisema .
Mhandisi kamwelwe
alisema mfumo huo utatumika kwa majaribio hadi kufikia juni mwaka huu na baada
ya hapo LATRA isitoe leseni kwa mmiliki ambaye hajajiunga na mfumo huu ili
kuhakikisha kila mmiliki a natumia mfumo huu.
"Kufikia
Septemba mwaka huu utekelezaji uanze kwa upande wa dalala nawaagiza kusimamia
kanuni kikamilifu hususan mfumo huu kila atakaye kuja kuchukua leseni lazima
aunganishwe na mfumo huu"alisema
Kwa upande wake
Mkurugenzi LATRA Gilliad Ngewe alisema kupitia mfumo huo watoa huduma
hawatodanganywa tena kuhusu mapato yao kwani kila abiria anapokatishwa tiketi
moja kwa moja hela ya mmiliki itakwenda benki na mwenyewe kupatiwa ujumbe kiasi
cha pesa na idadi ya wateja watakao hudumiwa kwa siku .
"Tajiri
atafunga mahesabu mwenyewe na si wakala tena ,tumejipanga kikamilifu kusimamia
utoaji huduma kwa mfumo huu na maafisa wetu watashirikiana na jeshi la polisi
kutoa elimu kuhakikisha wananchi wote wananufaika na mfumo huu na tutakuwa na
kituo cha huduma kwa wateja ambacho kitazinduliwa hivi karibuni watu kupitia
namba 0800110150 watapiga na kupata elimu juu ya mfumo huu"alisema.
Alisema mwananchi
kwa kutumia simu ya mkononi ataweza kununua tiketi ya basi analotaka aina ya
kiti na kupangiwa muda wa safari.
Alisema katika
ulipaji wa tiketi abiria ataletewa ujumbe kwenye simu ujumbe ambao utampa
maelekezo ya kufanya malipo na mara baada ya kukamilisha atapatiwa ujumbe
mwingine ambao utakuwa tiketi yake atakayolazimika kuitunza ili kuingia nayo
katika basi.
Pia kwa abiria
ambao hawatakuwa na simu janja hawatosumbuka Kwani watakapofika vituoni
watakatiwa tiketi hizo kwa kifaa maalumu POS .
Mbali na
hilo alisema abiria watanufaika zaidi Kwani kwa kutumia mfumo huo
watakuwa na uwezo wa kuchagua kituo cha kupanda basi pamoja na kushuka.
Mkurugenzi wa Imani
Class Amani Kaganda ambaye tayari ameanza kutumia mfumo huo kwa majaribio
alisema faida za mfumo huo ni mkubwa kwani mmiliki wa basi anajua fedha
alizoingiza kwa siku na kuanza kupanga matumizi yake .
"Fedha naipata
kwa wakati sisumbuki na watu kunipa hesabu pia nina uhakika na abiria
wanaoingia kwenye gari"alisema.
No comments:
Post a Comment