Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi. Evarist Ndikilo,
akizungumza wakati wa kikao maalumu cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya
Wilaya ya Bagamoyo kilichoandaliwa kwa
ajili ya kujadili majibu ya hoja za mkaguzi na mdhibiti wa hesabu za serikali
CAG (Picha na Victor Masangu).
Baadhi ya wakuu wa idara wakiwa wanafuatilia mkutano maaalumu wa baraza la madiwani katika halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo amabo ulianaliwa kwa ajili ya kupokea na kujadili majibu ya hoja kutoka kwa mkaguzi na mdhibiti wa hesabu za serikali kwa mwaka wa 2018/2019.
Baadhi ya madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo Mkoa wa Pwani wakiwa wameketi katika ukumbi wa mikutano kwa ajili ya kupokea taarifa na kujadili majibu ya hoja kutoka kwa mkaguzi na mdhibiti wa hesabu wa serikali.
Baadhi ya wakuu wa idara wakiwa wanafuatilia mkutano maaalumu wa baraza la madiwani katika halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo amabo ulianaliwa kwa ajili ya kupokea na kujadili majibu ya hoja kutoka kwa mkaguzi na mdhibiti wa hesabu za serikali kwa mwaka wa 2018/2019.
Baadhi ya madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo Mkoa wa Pwani wakiwa wameketi katika ukumbi wa mikutano kwa ajili ya kupokea taarifa na kujadili majibu ya hoja kutoka kwa mkaguzi na mdhibiti wa hesabu wa serikali.
Victor Masangu,
Bagamoyo
Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhandisi Evarist Ndikilo, amechukizwa na kuona miradi ya maendeleo ipatayo 42 yenye thamani
ya zaidi ya bilioni 1 katika halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo haijakamilika
kwa wakati hadi sasa kutokana na kuwepo kwa
baadhi ya watumishi na watendaji
kufanya kazi kwa mazoea na uzembe hali ambayo inasababisha hasara kubwa na kukwamisha juhudi za serikali ya awamu ya
tano katika kuwaletea wananchi maendeleo
hivyo wote watakaobainika kuhusika na ubadhilifu wowote wa fedha wachukuliwe
hatua kali za kisheria ili iwe fundisho kwa wengine.
Kauli hiyo aliitoa wakati wa mkutano maaalumu wa baraza la
madiwani wa halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo
wenye lengo la kupokea na
kujadili majibu ya hoja za mkaguzi na mdhibiti wa hesabu za serikali (CAG) kwa
kipindi cha mwaka wa hesabu kwa mwaka wa 2018/2019.ambapo pia ametoa muda wa
siku saba kwa uongozi wa halmashauri hiyo
kufunga hoja zote 38 ambazo
bado hazijakamilika hadi sasa kwani ili
kuendana na maagizo yaliyotolewa na serikali ya Mkoa.
Ndikilo alisema kwamba katika taarifa
amabayo imetolewa na mdhibiti na wa hesabu za erikali CAG imeweza kueleza kuwa
kuna baadhi ya miradi ambayo bado ijakamilika wakati fedha zake zimeshatolewa
hivyo kuna dalili za baadhi ya watendaji kutowajibika kikamilifu katika
uetekelezaji wa majukumu yao.
“Fedha zimetolewa kabisa shilingi bilioni 1 na milioni 24
lakini mimi nashangaa miradi 42 bado haijakamilika kwa wakati kabisa hii kwa
weli sio sahihi hata kidogo hapa inatakiwa ndugu zangu madiwani wa baraza hili
kuangalia kwa makini maana hii miradi ni mingi kwa hiyo mimi ninachokiomba
miradi hii iweze kukamilika kabisa kwa wakati na kwa wale watumishi ambao
watakuwa wamehusika katika uzembe huu ni lazima wachukuliwa hatua kali z
akisheria.
Aidha Mkuu huyo aliongezea kuwa kwa sasa inatakiwa hoja zote
ambazo ziliitajika kukamilishwa kwa kipindi hiki ni lazima zifanyiwe kazi
haraka iwezekanavyo maana ni agizo ambalo lilishatolewa na serikali ya Mkoa kwa
hiyo mimi naagiza ndani ya siku saba kwa maana ya wiki moja hoja hizi 38 na
kipindi cha mwak 2018/2019 ni lazima zikamilika pamoja na zile hoja nyingine za
miaka iliyopita.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Zainabu Kawawa
amesema licha ya halmashauri hiyo kupata hati safi kwa mfululizo kuanzia
kipindi cha kuanzia mwaka 2015 hadi 1019 lakini watendaji na watumishi wanapaswa
kubadilika kwa kutekeleza majukumu yao
kwa weledi hasa katika suala zima la
kudhibiti mianya ya upotefu wa mapato pamoja na kusimamia kikamilifu fedha zinazotolewa katika miradi ya
maendeleo.
Kawawa alibainisha kwamba katika halmashauri ya Wilaya ya
Bgamoyo kumekuwepo na changamoto mbali mbali katika suala zima la ukusanyaji wa
mapato hivyo kunahitajika juhudi z amakusudi katika kuhakikisha mashine ambazo
zinatumika katika ukusanyaji wa mapato hayo zinakuwa zinawashwa kwa lengo la
kuweza kuongeza makusanyo tofauti na ilivyokuwa kwa sasa.
“Hii hali ya ukusanyaji wa mapato katika halmashauri ya
Wilaya ya Bgamoyo sio mzuri ndio ni kweli tumefnikiwa kupata hati safi kwa
awamu nne mfululizo lakini sisi kama viongozi ni lazima tufuatilie kwa umakini
kuhusiana na ukusanyaji w amapato haya
mbali mbali maana nasikia kuna mashine nyingine zinakuwa zimeimwa kwa
kipindi cha muda mrefu sasa hii ni hatari sana lazima mapato yetu yapotee tuu
kutokana na uzembe wa baadhi ya watu,”alisema Kawawa.
Naye Mkaguzi wa Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi na Udhibiti wa Hesabu za Serikali (CAG) wa Mkoa wa Pwani Mwajuma Kwipunda alibainisha kwamba
halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo kwa kipindi cha mwaka 2018/2019 licha ya
kuwepo kwa mapungufu ya kutokamilisha mapendekezo kwa wakati imefanikiwa kupata
hati safi.
Katika hatua nyingine Mwenyekiti wa halmashauri hiyo
amefarijika kupokea hati safi kwa mara ya nne mfululizo na kuahidi kuyafanyia
kaiz kwa vitendo maagizo yote nane
ambayo yametolewa na Mkuu wa Mkoa kuhusina na mambo mbali mbali katika kusimamia utekelezaji wa miradi ya
maeneleo pamoja na utekelezaji wa hoja ambazo bado hazijafanyiwa kazi.
Halmashauri ya Wilaya
ya Bagamoyo iliyopo Mkoa wa Pwani licha ya kupatiwa hati safi mfululuzo kuanzia
kwa kipindi cha mwaka 2018 hadi 2019 kutoka kwa
mkaguzi na mdhibiti wa hesabu za serikali (CAG) lakini bado inakabiliwa
na changamoto mbali mbali katika masuala ya ukusanyaji wa mapato pamoja na
kutokamilisha kwa baadhi ya miradi ya maendeleo kwa wakati.
No comments:
Post a Comment