Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri
(kulia) akimkabidhi jana Mkuu wa Wilaya ya Igunga John Mwaipopo mmoja ya gauni likiwa
ni msaada kutoka Shirika la World Vision kwa ajili ya kutumiwa na watoa huduma
wakati wa kumhudumia mgonjwa wa Covid-19.
(Picha na Tiganya Vincent).
(Picha na Tiganya Vincent).
Na Tiganya Vincent, Tabora
SHIRIKA la World Vision
Tanzania limekabidhi vifaa vya thamani ya shilingi milioni 17.1 vya kudhibiti
virusi vya Corona vinavyosababisha ugonjwa wahoma kali ya mapafu ya Covid -19
kwa Mkoa wa Tabora.
Msaada huo umekabidhiwa leo
mjini Nzega na Meneja wa Kanda wa Shirika World Vision John Masenza kwa Mkuu wa
Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri.
Alitaja msaada huo
unajumuisha glovu boksi 990, magauni ya wahudumu wa afya ya kuwafaa wakati wa
kuwahudumia wagonjwa 80 , lita 290 ya vitakasa mikono na vipasa saui kwa ajili
ya utoaji wa elimu kujikinga na corona 22.
Masenza alisema msaada
huo utagawanywa kwa Halmashauri zote nane za Mkoa wa Tabora ili ziwaweze watoa
huduma kusaidia katika mapambano dhidi ya Covid-19.
Alisema msaada mwingine
ambao ni barakoa kwa ajili ya huduma za upasuaji ziko njia na zitarajiwa
kuwakabidhiwa baada ya kuwasili.
Akipokea msaada huo Mkuu
wa Mkoa wa Tabora Mwanri alilishukuru shirika la World Vision kwa kuunga mkono
juhudi za Serikali za kukabiliana na kudhibiti ugonjwa wa Covid -19.
Alisema msaada huo umekuja wakati
muhimu ambapo Taifa liko katika vita ya kudhibiti ugonjwa wa Covid- 19
usiendelee kusambaa.
Mkuu huyo wa Mkoa alisema wadau wote Mkoani
humo wanapaswa kuungana katika vita ili hatimaye waweze kuushinda ugonjwa wa
Covid-19.
Alisema msaada huo walioupokea baada
ya kudhibitishwa na wataalamu wa sekta ya afya kuwa ziko vizuri zitagawanywa
katika Wilaya zote za Mkoa wa Tabora kwa ajili ya kuwasaidia watoa huduma za
afya ambao wanasaidia kukabiliana na ugonjwa wa Covid-19 na watu wengine ambao
hajiwezi.
Mkuu huyo wa Mkoa alitoa wito kwa
wadau wengine wanaoendesha shughuli zao ikiwemo za biashara na kutoa huduma
mbalimbali kuendelea kushirikiana na Serikali katika mapambano dhidi ya janga
la Corona.
No comments:
Post a Comment