HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

June 02, 2020

IGP SIRRO AWATAKA VIJANA KUACHA KUTUMIWA NA WANASIASA

Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchin IGP Simon Sirro amewataka vijana kuacha kutumiwa na wanasiasa wachache wanaotaka kujinufaisha kisiasa au kujipatia umaarufu na badala yake watimize wajibu wao wa kupiga kura.

IGP Sirro amesema hayo leo akiwa mkoa wa Kipolisi wa Tarime/Rorya mkoani Mara ambapo alifanya ziara ya ukaguzi na kuzungumza na Polisi kata wa mkoa huo huku akiwataka baadhi ya wananchi wa mkoa wa Mara kuacha kujihusisha na wizi wa mifugo pamoja na mila potofu na zilizopitwa na wakati hasa vitendo vya ukeketaji ambalo ni kosa la jinai.

Aidha, IGP Sirro ameendelea kuwaasa viongozi wa dini kuacha kujihusisha na masuala ya kisiasa na badala yake wafanye kazi zao za kidini.
 IGP SIMON SIRRO, MKUU WA JESHI LA
POLISI NCHINI.


No comments:

Post a Comment

Pages