HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

June 12, 2020

KATIBU MKUU MALIASILI NA UTALII AKAGUA NYAYO ZA ZAMADAMU WA KALE ZAIDI DUNIANI ENEO LA LAETOLI

Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Prof. Adolph Mkenda, ameiagiza Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro, kuhakikisha inakamilisha mchakato wa kuzihifadhi kisayansi nyayo za zamadamu wa kale zaidi duniani, zilizopo katika eneo la Laetoli ndani ya Hifadhi, ambazo kwa sasa bado zimehifadhiwa chini ya mawe na udongo maalumu,hali ambayo haiwapi fursa ya kuziona nyayo hizo moja kwa moja,watalii wanaofika katika eneo hilo la kihistoria duniani.
 Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii, Prof. Adolph Mkenda, akikagua Nyayo za Zamadamu wa kale zaidi duniani katika eneo la Laetoli lililopo ndani ya Hifadhi ya Ngorongoro mkoani Arusha, ambazo zinaamika kwa na miaka milioni tatu nukta sita tangu binadamu wa kale alipoanza kutembea kwa miguu miwili.
Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Prof. Adolph Mkenda, akitoa maelekezo kwa watumishi wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro ya kuhakikisha mchakato wa kuhifadhi kisayansi zaidi Nyayo za Zamadamu wa kale zaidi duniani katika eneo la Laetoli lililopo ndani ya Hifadhi ya Ngorongoro mkoani Arusha, ambazo zinaamika kwa na miaka milioni tatu nukta sita tangu binadamu wa kale alipoanza kutembea kwa miguu miwili. (Na Mpiga Picha Wetu).

No comments:

Post a Comment

Pages