KAMPUNI
ya mawasiliano inayoongoza kwa kutoa huduma za kidigitali nchini, Tigo Tanzania
imezindua huduma mpya ya Tigo Rusha iliyoboreshwa.
Hayo
yamesemwa na Kaimu Mkuu
wa Kitengo cha Biashara wa Tigo Tanzania, David Umoh wakati akizungumza na
waandishi wa habari kwa njia ya Zoom ambapo aliweka bayana kuwa huduma hiyo inamuwezesha
mteja wa Tigo kununua muda wa maongezi pamoja na vifurushi kutoka katika maduka
ya Tigo ya rejareja yanayotambuliwa na Tigo Tanzania.
“Huduma
hii ya Tigo Rusha iliyoboreshwa itatolewa katika mtandao wa mauzo wa
Tigo ikiwa ni pamoja na maduka ya Tigo, mawakala wa Tigo Pesa, wauzaji wa
kujitegemea, pamoja na vituo vya mauzo nchi nzima. Huduma hii itaongeza wigo wa
namna ya kuongeza salio kwa wateja,” alisema.
Umoh,
alisema, Tigo ikiwa moja ya kampuni inayoongoza kwa huduma za kidigitali, wamejizatiti
kuimarisha na kubuni njia zenye kuleta unafuu na zenye chaguzi nyingi ili
kumpatia mteja fursa ya kuchagua huduma inayoendana na mahitaji yake kulingana
na sehemu aliyopo na muda husika.
“Tunafanya
maboresho haya ili kuendana na kasi ya mabadiliko ya kiteknolojia na maisha kwa
ujumla. Wateja wetu wakae mkao wa kula kwamba sasa wataweza kununua muda wa
maongezi pamoja na vifurushi kutoka kwenye maduka yetu pamoja na wauzaji
wengine wanaotambuliwa na Tigo nchi nzima,” alisema.
Kaimu
mkurugenzi huyo alisema Tigo Rusha haina changamoto za kuharibika kwa karatasi
ya vocha za kukwangua, lakini pia huduma hii inampunguzia adha mteja kutembea
na kadi za vocha pindi anapohitaji kuongeza salio kwenye simu yake.
“Tigo Rusha inawapa wateja wetu thamani ya pesa zao kwa
maana huduma hii ni rahisi sana kutumia, salama na ya uhakika. Kila mteja wa
Tigo atakeyenunua salio au kifurushi chochote kupitia huduma hii ya Tigo Rusha anapewa
zawadi ya nyongeza,” anaeleza Umoh.
“Napenda
kuwahakikishia wasambazaji wetu wote wa vocha za kukwangua kwamba hii ni fursa
mpya ya kuongeza kipato, hivyo ni fursa pia kwao kukua pamoja na Tigo na kama
kampuni tutaendelea kuwaunga mkono wasambazaji wote wa vocha hizo za kukwangua
kote Tanzania,” alisema Umoh.
Alisema
wateja wote wa Tigo wanashauiriwa kununua muda wa maongezi pamoja na vifurushi
kutoka kwa wauzaji na mawakala wa Tigo Rusha ambao wanapatikana katika maeneo
yote nchini Tanzania.
Kwa
upande wake Mkuu wa Masoko Tigo, William Mpinga alisema huduma hiyo ya Tigo
Rusha itakuwa endelevu hivyo kuwataka watumiaji waitumie.
No comments:
Post a Comment