HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

July 19, 2020

Benki ya CRDB kusaidia upasuaji wa moyo kwa watoto 100 JKCI

 Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Benki ya CRDB, Tully Mwambapa (wa pili kushoto) na wafanyakazi wengine wa Benki hiyo wakikimbia mbio za km 10 wikiendi hii ikiwa ni sehemu ya maandalizi kuelekea mbio za hisani za "CRDB Bank Marathon" zinazotarajiwa kufanyika tarehe 16 Agosti, 2020 kwa ajili ya kukusanya fedha kusaidia watoto wenye uhitaji wa upasuaji wa moyo katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete.
Wafanyakazi wa Benki ya CRDB wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kukimbia km 10 ikiwa ni sehemu ya maandalizi kuelekea mbio za hisani za "CRDB Bank Marathon" zinazotarajiwa kufanyika tarehe 16 Agosti, 2020 kwa ajili ya kukusanya fedha kusaidia watoto wenye uhitaji wa upasuaji wa moyo katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete.


 Na Irene Mark

BENKI ya CRDB imeandaa mashindano ya riadha yenye lengo la kukusanya fedha kwa ajili ya kusaidia upasuaji wa moyo kwa watoto 100 waliopo katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) jijiji Dar es Salaam.

Mashindano hayo yaliyobeba kaulimbiu isemayo ‘Kasi isambazayo tabasamu’ yatafanyika Agosti 16,2020 yakihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa kitaifa wakiongozwa na Makamu wa Rais, Mama Samia Suluhu.

Akizungumzia mbio hizo mwishoni mwa wiki mbele ya wanahabari ofisini kwake jijiji Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Benki ya CRDB, Tully Esther Mwambapa, alisema lengo ni kuokoa maisha ya watoto 100 kati ya 511 wasio na uwezo wanaosubiri kufanyiwa upasuaji wa moyo kwenye taasisi hiyo.

Alisema ushiriki wa mashindano hayo ni Sh.30,000 wakitarajia kupata washiriki 4,000 kutoka ndani na nje ya nchi  wataochangia matibabu ya watoto hao wakishirikiana na wadau mbalimbali.

“Benki ya CRDB inasaidia jamii kwenye maeneo matatu ambayo ni Afya, Elimu na Mazingira tumeanza na afya kwa kuwasaidia watoto hao na huu ni muendelezo tutafanya hivi kila mwaka.

“...Nikatika kurudisha kwa jamii. Tunaakika jogging clubs mbalimbali kushiriki nasi. Tukimbie kwa afya huku tukiokoa maisha ya watoto wetu wa kitanzania.

“Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mtendaji wa JKCI gharama ya upasuaji wa moyo kwa mtoto mmoja ni kati ya Sh. Milioni mbili hadi Sh. Milioni20 watoto wanaosubiri huduma hiyo ni 511 sisi tumeanza kusaidia hawa 100 naamini wengine pia wataunga mkono jambo hili,” alisema Tulli.

Kwa mujibu wa mkurugenzi huyo, washiriki wanaweza kujisaijili kwa njia rahisi ya mtandao wa CRDB Marathon na kulipia kwa Simbanking, matawi ya Benki ya CRDB, mawakala wa Fahari Huduma na mitandao ya simu.

Tulli alibainisha kwamba watu wa mikoani wanaweza kushiriki kupitia kwenye matawi ya Benki ya CRDB popote walipo.

No comments:

Post a Comment

Pages