HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

July 16, 2020

CHADEMA VUNJO WAMCHAGUA GRACE KIWELU KUGOMBEA UBUNGE

Aliyekuwa Mbunge kupitia Viti Maalumu Chadema Mkoa wa Kilimanjaro Grace Kiwelu akipita mbele ya Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Chama hicho jimbo la Vunjo kuomba ridhaa ya kugombea Ubunge katika jimbo hilo.
Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo Chadema ,mkoa wa Kilimanjaro Michael Kilawila akizungumza wakati wa uchaguzi huo.
Kura zikihesabiwa mara baada ya wajumbe wa mkutano huo kukamilisha zoezi la upigaji kura ,wagombea wa nafasi hiyo Grace Kiwelu (Kulia ) na mshindani wake Collins aliyewakilishwa katika uchaguzi huo wakipokea karatasi za kura wakati wa uchaguzi huo.katikati ni msimamizi wa Uchaguzi Elisa Mungure.

Na Dixon Busagaga ,Vunjo

MJUMBE wa Mkutano Mkuu wa Cha Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Grace Kiwelu ameshindwa kuzuia hisia zake na kuangua kilio baada ya kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi wa kumpata Mwakilishi wa Chadema katika nafasi ya Ubunge katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba mwaka huu.

Kiwelu aliangua kilio hicho wakati wa  matokeo ya uchaguzi huo wa kura za maoni yalipotangazwa Jana msimamizi wa uchaguzi huo,Elisa Mungare, alisema kwa mujibu wa kura zilizopigwa  ambazo ni 84,Kiwelu alichaguliwa kwa kura 80 sawa na asilimia 95 huku mgombe mwenzake Colin Msofe akiambulia kura 4.


"Namtangaza Grece Kiwelu kupewa ridhaa na wajumbe Hawa kupeperusha bendera ya CHADEMA katika Jimbo hili hii Ni baada ya kushinda kura za maoni baada ya yeye kupata kura 80 dhidi ya mgombea mwenzake ambaye amepata kura 4"alisema

Mbali na Kiwelu kuchaguliwa kuwa mgombea wa ubunge katika Jimbo hilo pia Baraza la wanawake wa Jimbo la Vunjo walimchagua kuwa mgombea wa ubunge wa viti maalumu wa Chadena wa mkoa wa Kilimanjaro.

"Kiwelu amepata kura 25 na Haziza Mohamed  5  Kati ya kura 30 zilizopigwa na wajumbe hivyo kulinga na mamlaka niliyopewa namtangaza Kiwelu kuwa mgombea wa viti maalumu mkoa wa Kilimanjaro"alisema


Akizungunza Mara baada ya zoezi Hilo kumalizika, Grece Kiwelu, alisema anawashukuru wajumbe wa mkutano huo kwa namna walivyomuamini na kumchagua kuwa mgombea wa ubunge wa Jimbo Hilo na mgombea wa ubunge wa viti maalumu mkoa wa Kilimanjaro.

"Nimeteuliwa kugombe ubunge wa Jimbo hili nauhakika nitaipeperusha bendera ya Chadema vizuri ....Jimbo la Vunjo katika uchaguzi wa Mwaka 2015 hatukuweka mgombea Ila Sasa nipo Mimi nitapambana na CCM"Alisema

Aidha alisema dhana ya kutawala kwa mfumo dume uchagani haipo na kwamba anaamini yeye Kama mwanamke anauwezo wa kuliongoza Jimbo Hilo na kuleta maendeleo katika nyanja zote. 

"Nimelia machozi ya furaha naamini wajumbe wameniamini na nitahakikisha Jimbo hili linakuwa na maendeleo makubwa"alisema

No comments:

Post a Comment

Pages