HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

July 14, 2020

HALMASHAURI YA BUKOBA YAFANIKIWA KATIKA SUALA LA LISHE


Na Lydia Lugakila, Bukoba

Halmashauri ya wilaya ya Bukoba Mkoani Kagera imeendelea
kushika nafasi ya kwanza katika kufanikisha suala la lishe ikiwa ni pamoja na kununua mizani 4 ya kisasa inayoshauriwa na shirika la afya duniani WHO.

Kauli hiyo imetolewa na Afisa Lishe wa Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba mkoani Kagera, Desdery Karugaba, wakati akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa shughuli za lishe, kutoka idara ya afya katika kikao cha kamati ya lishe cha robo ya nne kuanzia mwezi Aprili hadi juni mwaka huu, kilicholenga kujadili masuala ya lishe.

Karugaba amesema kuwa kwa namna ya kipekee anatoa
shukrani za dhadi kwa niaba ya kamati kwa ofisi ya mkurugenzi mtendaji wa halmashauri hiyo Solomoni Kimilike kwa namna alivyoiwezesha halmashauri hiyo kutekeleza mkataba ya utendaji kazi wa shughuli za lishe, uliosainiwa na wakuu wa mikoa na waziri wa wa nchi ofisi ya Rais na baadae kusainiwa na wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya chini ya uangalizi wa wakurugenzi.

Amesema kuwa mkataba huo ulilenga kuboresha utekelezaji wa afua za lishe baada ya kuona kwamba zilikuwa nyuma sana.
 
Amesema kuwa tangu mkataba huu usahiniwe jumla ya
tathimini 4 zimefanyika katika halmashauri 8 za mkoa wa
kagera ambapo kila robo inafanyika tathimini ambapo
Halmashauri hiyo imekuwa ya kwanza mara tatu kati ya mara nne, zilizofanyika kwa kununua mizani 4 ya kisasa
inayoshauriwa na shirika la afya duniani WHO. 

Mizani hiyo imegawiwa katika vituo vya kutolea huduma za afya kikiwemo kituo cha Katoro, Ruhunga na hospitali ya wilaya ya Bukoba huku akiahidi kuendelea kupata ushindi.
 
Karugaba amesema kuwa licha ya kufanya vizuri katika masuala ya lishe bado kuna changamoto mbali mbali zinawakabili ikiwa ni pamoja na vifaa vya kufanyia tathimini hali ya lishe hasa katika kiashiria cha udumavu.
 
Katika hatua nyingine afisa lishe huyo amewataka wahudumu wa afya wilayani humo kuhakikisha wanatoa elimu katika shule za binafsi mkoani Kagera, kutumia chumvi ya madini chuma na kuachana na chumvi ya mawe jambo linaloweza kusababisha suala la udumavu kwa watoto wanaopelekwa shuleni wakiwa katika umri mdogo.

Kwa upande wake mwenyekiti wa kikao hicho ambaye pia ni
mkuu wa idara ya afya wilayani humo Bi Bandioti Gavyole amewahimiza wahudumu wa afya kuendelea kusisitiza suala la lishe shuleni ikiwa ni pamoja na kuwakumbusha wanafunzi kunawa mikono kwa kujikinga na virusi vya Corona.

No comments:

Post a Comment

Pages